Mkurugenzi
Mtendaji wa MKUKI NA NYOTA PUBLISHERS Bw. Walter Bugoya akitoa neno wakati wa
uzinduzi wa kitabu cha 'FURAHA HUJA ASUBUHI' (JOY COMES IN THE MORNING)
kilichoandikwa na Hopolang Phororo kinachozungumzia Mateso na manyanyaso ya
wasichana wadogo wakati wa malezi yao na haki ya msingi ya jinsia ya kike katika
jamii.
Mmoja
wa washiriki wa uzinduzi huo Bi. Chansa Kapaya akitoa neno la shukrani wakati wa
uzinduzi wa kitabu cha Hopolang Phororo na haki za msingi za wanawake wanaokutwa
na matatizo ya unyanyasaji wa Kijinsia Tanzania"
Mtunzi
wa Kitabu cha 'JOY COMES IN THE MORNING' Bi. Hopolang Phororo akielezea simulizi
ya kweli iliyomkuta kama mwathirika wa unyanyasaji wa Kijinsia wakati wa
usichana wake na moyo, uvumilivu aliokuwa nao wa kuweka uzoefu huo katika
maadishi ili jamii ijifunze na madhara ya unyanyasaji wa Kijinsia unaokua kwa
kasi nchini Tanzania"
Mgeni rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Fatma
Mrisho akitoa nasaha zake wakati uzinduzi rasmi wa kitabu hicho jijini Dar es
Salaam. Alisema 66% ya wanawake na 20% ya wanaume nchini wameshawahi kukutwa na
majanga ya unyanyasaji wa Kijinsia katika maelzi yao ambapo kwa sasa Dar es
Salaam na Mbeya zinaongoza"
Mgeni rasmi Dkt. Mrisho na Mtunzi wakionyesha Kitabu
kwa wageni waalikwa na waandishi wa habari. Kitabu hiki kinapatikana katika
Maduka ya MKUKI NA NYOTA PUBLISHERS yaliyopo jijini Dar es Salaam kwa gharama
ya shilingi 10,000/=.
Jopo
la Wataalam wa Mambo ya Jinsia Tiba na Vitabu wakiwa kwenye picha
ya pamoja"
Mkurugenzi
wa MKUKI NA NYOTA PUBLISHERS Mzee Bugoya akibadilishana
mawazo na Dkt. Mrisho
pamoja na Bi. Kapaya wakati wa uzinduzi"
Baadhi
ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa kitabu cha 'JOY COMES IN THE
MORNING' uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment