Ndugu zangu Watanzania wenzangu ' Wakati wetu ndiyo huu 'wakukuwepo na Rais wetu Macho kwa macho ''Sasa anza kujipanga kwa maswali yako na vile vile kwa usafiri ,maana hakuna mabasi ya Bure'' Ila kuna Ndege za Bure zitakazo pitia Detention UK, Yarl's Wood fasta fasta'na Kushusha Watanzania wote ili waweze kuwapa support wale Watanzania wenzao waliomo mle ndani 'Mbuta nanga''JAMANI WAPO WENGI NA SYO MMOJA AU FAMILIA MOJA MLE ,YANI AMINI USIAMINI''IS NOT A JOKE'' Tuwawekeni katika sala,Wote waliopo mle wa Nchi mbali mbali Mungu awasaidie waweze kupata wanachokihitaji which is stay in UK'' AMEN'' Anyway''sasa shuka chini soma yalokuleta hapa maana kichwa cha habari ya hii Blog ndichokimekuleta hapa eee''
Ubalozi wa Tanzania London - Uingereza, unafuraha ya kuwatangazia Watanzania wote waishio Uingereza kuwaMhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atakutana na Watanzania siku ya Jumapili tarehe 30 Machi 2014.
Mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Sattavis Patidar Centre, Forty Avenue, Wembley Park, London, Middx, HA9 9BE, kuanzia saa 10 jioni (16:00).
Katika Mkutano huo, Mhe.Rais Kikwete atazungumzia maendeleo ya nchi yetu na pia kutumia fursa hiyo kusikia masuala yanayogusa maslai ya wanadiaspora.
Mhe. Rais atakuwa nchini Uingereza kuanzia tarehe 30 Machi hadi 2 April 2014 kwa ziara ya kikazi kwa mwaliko rasmi wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Mhe. David Cameron.
Ubalozi unapenda kuchukua fursa hii kuwaomba Watanzania wa maeneo ya Uingereza na nchi jirani kujitokeza kwa wingi kumkaribisha Rais kwenye Mkutano huu adimu.
Kwa Taarifa zaidi:
Simu: 0207 569 1470
Ahsanteni sana- Ubalozi wa Tanzania – London
No comments:
Post a Comment