Ona Hasara hii 'sasa hapa paonekana kama ni makazi ya Mtu 'kwa kweli ni hasara kubwa sana kwa Mfanya biashara yoyote'' Poleni sana Ndugu zetu tupo pamoja ' |
Ona hasara Hiyo ni Nyumba ya mtu na pia maeneo yote ni ya shughuli za watu pita pita za kujitafutia riziki zao na watoto kwenda shule'' Poleni sana Ndugu zetu ,tupo pamoja'' |
Ona kuleee kwa mbali mnaweza kuona Nyumba za watu yani maji ni karibu kufuka mapawa kabisa''' Mungu wangu azidi kuwabariki na kuyakausha maji na mvua kuzisimamisha kwa sasa'' poleni sana ndugu zetu tupo pamoja'' |
Uwiii''si niajabu hii,wananchi waonekana wakisaidia Ila kwa njia hii naona hawatafika mbali ,Serekali yetu haina vyombo maalum vya kushimbua mitaro na mashimo hayo yaliyoziba jamani'' I think huziba kwa sababu ya takataka nazo zinazotupwa Ovyo ovyo '' ni wajibu wetu Wananchi Mnaoishi huko Nyumbani kwa sasa kufanya usafi kuzoa taka taka kabla hazijanyesha mvua kama hizi na kusababisha kuziba mashino hayo' Na Serekali inatakiwa kuwapa kazi vijana waliozaga zagaa mitaani bila kazi na kuweza kupewa kazi hiyo ''kama wanavyo fanya huku Ulaya'' Unakuta Barabara na mitaa inafagiliwa kila Usiku ''na hao wafagiaji wengine hawalipwi huwa ni adhabu waliyopewa mahakamani kwa makosa madogo dogo ,wao huwapa kazi za kusafisha mitaa na pia kukata nyasi na kukata miti'' huku wakipewa vyombo hivyo kwa ajili ya safisha safisha'' na huko Nyumbani tunaweza kufanya hivi ''Ili kujiandaa kwa Mvua za wakati wowote'' Hayo ni maoni yangu tu''kwani najua how it feel '' Poleni sana Ndugu zetu Tupo pamoja'' |
Hasara hasara hasara kubwa ' Ndugu zangu Watanzania hasa Tuishio hapa UK ,Mimi sioni kama tutashindwa wengi wetu kutoa hata hiyo £10 pounds kuwasaidia hawa wenzetu 'yani hatutashindwa kabisa ,kumbukeni hawa ni wenzetu na aghalau sie tupo huku majuu ,tunaweza kuwasaidia kwani wengi wetu tukipunguza bajeti yetu ya msosi hata wa mara mbili kwa siku na kula mara moja kwa siku ,hatuwezi kufa njaa na wenzetu wataweza kupata hata huo mlo wa mara moja kwa siku na pia kuwasaidia kuweza kujenga maisha yao tena 'kwa kidogo tutakacho toa kwa wengi wetu ,which hadi sasa hivi sijui Idadi ya watanzania waliopo UK ni wangapi ,lakini kwa Uwe umati wa mamia ya Watanzania waliojitokeza Majuzi kukutana na MH.Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipokutana nasi on 30.3.2014 Mwezi uliopita,Tukijitokeza hivyo tena au hata kama hatuwezi kufika na kuweza kutoa hiyo £10pounds 'itasaidia sana ''hata £7.000 Pounds zinaweza kupatikana tena bila shida yoyote'' Mimi naona ni jambo la Umoja na Upendo ''na Vile vile tukienda na ule msemo wetu wa kutoa ni moyo na siyo utajiri ''tutaweza' Tusitejemee Mfuko wa serikali ''Serekali pia ni Sisi wenyewe 'hasa tuliobahatika kukuwepo huku majuu'' DIASPORA COMMUNITY ,UK ,LONDON MPOOO'' I DO THINK ITAKUWA POWA SANA MKIWEZA KUIFANIKISHA HARAMBEE HII''MIMI NIPO TIYARI NA £10 YANGU '' HAVE YOUR SAY MY TANZANIA NDUGU'' Ni hayo tu ''Mungu azidi kutubariki na tukumbukeni ''Maisha ni kusaidiana na siyo kutengana'' Flora Lyimo Fashion Police Blog |
No comments:
Post a Comment