FLORA LYIMO AKA MBUTA NANGA NA MHESHIMIWA RAIS WETU KIKWETE
Na mimi Flora Lyimo ninapenda kusema ASANTE SANA RAIS WETU ''IM SO PROUD OF YOU ' Umetuongoza ipasavyo na I WISH UNGEZIDI KUTUONGOZA MILELE'' RUWA MANGI'' Mungu akupe afya njema na miaka mingi isiyo hesabika kabisa'' AMEN'
AIKA MBEE KANYI NA UKAE NA RUWA''
Na Bashir Nkoromo, theNkoromo Blog
Wasanii wa fani mbalimbali jana kuanzia jioni walijumuika na Rais Jakaya Kikwete katika chakula cha jioni, kwa ajili ya kuagana naye, kufuatia kukaribia kumaliza mda wake wa urais.
Katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, pamoja na Rais Kikwete, ilihudhuriwa pia na Mgombea mteule wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Rais Jakaya Kikwete alisisitiza kuwa wasanii ni watu muhimu ambao kazi zao zinapaswa kulindwa ili ziwanufaishe kama ilivyo kwa wasanii wengine duniani kama walioko nchi kama za Marekani.
Rais Kikwete aliahidi kuendelea kusaidia juhudi za kuwafanya wasanii waishi maisha yaliyo bora kwa kupata kipato kinacholingana na kazi zao hata akishastaafu nafasi yake ya urais.
Ili kutekeleza azma yake hiyo, Rais Kikwete aliahidi kuwa mlezi wa wasanii ili kuwewezesha masuala yao mengi yapige hatua zaidi.
Mapema wasanii walimtawaza Rais Kikwete kuwa Shujaa wao, na kumtunuku picha maalum iliyonakshiwa karibu majina ya wasanii wote nchini, Picha hiyo alikabidhiwa na Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Nikki wa Pili ambaye kabla ya tukio hilo, alieleza jinsi tasnia ya sanaa, inavyochangia pato la taifa na changamoto zinazowakabili wasanii.
Katika hafla hiyo, Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye walichangamsha ukumbi, baada ya kupanda jukwaani na kuzicharaza ala za muziki kwa umahiri mkubwa.
Dk. Magufuli aliamsha hoihoi ukumbini kwa kuzicharaza tumba, huku Napa akicharaza gita zito la Bess, na wote kuunogesha moja ya nyimbo za zamani, wa DDC Mlimani Park ulioimbwa na msanii, Recho.
Baadhi ya wasanii wengine waliotumbuiza ni Farid Kubanda (Fid Q), Shakila, Rud, Jose Mara.
---------------------------------
HABARI KATIKA PICHA

Rais Jakaya Kikwete akiingia katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, kuhudhuria chakula cha jioni, kilichoadaliwa kwa ajili ya Rais Kuagana na wasanii wa fani mbalimbali hapa nchini, jana usiku. Pamoja naye ni Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Bumbuli, January Makamba.
---------------------------------
HABARI KATIKA PICHA
Rais Jakaya Kikwete na viongozi aliofuatana nao wakiwa wamewasili ukumbini na zifuatazo ni picha mbalimbali za wasanii waliohudhuria ukumbini
Kassim Mponda akiwa na wenzake maarufu
Mzee Kingi Kikii akiwa na wenzake maarufu
Rais Kikwete akimsalimia Mzee Yusuf kwa furaha
Akimsalimia pia mke wa Mzee Yussuf
Mzee Yussuf akapata fursa ya kuteta jambo Rais Kikwete
Wasanii wakijipiga picha kwa simu na Rais Kikwete wakati akiwasalimia
Rais Kikwete akiwasalimia kwenye meza ya Kina Baba Zoro
Rais Kikwete alifurahi kiasi cha kukumbatiana na baadhi ya wasanii, kama alivyofanya hapa
Akafika hadi meza aliykuwepo Madam Rita wa Bongo Star Search
Nao wakapata fursa ya kujipiga picha na Rais kwa kutumia simu yao
Rais akafika hadi kwa Juma Kaseja
Salam zikaendelea
Rais Kikwete akajitahidi kusalimia kila mmoja na zifuatazo ni picha mbalimbali za wasanii wakiwa kwenye meza zao
Wasanii wakiwa wameketi kwa utulivu mezani
Bi Shakila akiwa na mwenzake
Fid Q akiwa ndani ya nyumba
Wengine wakiwa katika nyuso za kutafakari hali ya mambo
Wengine wakiendelea na vinywaji
Wasanii wakijichanganya bila kujali fani zao
Ally Chocky (kushoto) ndani ya nyumba
Diamond Platinum akisalimia wenzake baada ya kuingia ukumbini
Jay B (kushoto) pia ndani ya nyumba
Baadhi ya wakurugenzi wa vyombo vya habari wakiwa ndani ya nyumba. hapo kuna Benny Kissaka (kushoto) na kulia ni Danny Chongolo
Rey naye ukumbini
Mzee Yussuf na mkewe wakiwa ndani ya nyumba
Kina Juma Kaseja ndani ya nyumba
Msanii Rubby akiimba wimbo maalum wa kuisifu Tanzanaia
Fid Q akiimba kutumbuiza ukumbini
Jose Mara akiimba wimbo wa Mbaraka Mwishehe wa kuisifia Morogoro
Diamond akitoa tamko kuhusu tasnia ya Sanaa, alisema, kabla ya umaarufu aliwahi kudandia kampeni za CCM kutoka Mwanza hadi Dar, hadi akatambuliwa
Rais Kikwete uso kwa uso na Msanii na Msanii King Majuto
Bi Shakira akiimba wimbo Macho yanacheka Moyo unalia
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Magufuli akizicharaza tumba, huku Nape akicharaza Bess
Recho akiimba wimbo wa Sikinde
Msanii akimtunza Dk. Magufuli Dola za marekani baada ya kuvutiwa anavyocharaza tumba
Jay B na Mwana FA wakiwa wamekaribishwa kuketi meza kuu
Bushoke akiimba wimbo wake wa maarufu wa kunyanywaswa na mke
Shughuli hiyo ikamfikisha Hussein Bashe katikati ya Nape na Kinana
Kinana akimshauri jambo Bashe
Rais Kikwete akipata picha na Fid Q
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni akisakata mzuziki na Madam Rita
Rais Kikwete akisakata muziki katikati ya wasanii
Nikki wa pili akitoa maelezo kabla ya kumkabidhi Rais Kikwete picha maalum
Rais Jakaya Kikwete akikabidhiwa picha maalum yenye majina ya wasanii karibu wote, kutoka kwa Nikki wa Pili. Kulia ni Fid Q. Picha zote na Bashir Nkoromo.
ASANTENI WASANII NA PIA ASANTENI KWA WARUSHAJI WA PICHA ZOTE'
No comments:
Post a Comment