*MKILETEWA HAPA NA MISS FB FLORA BAHATI LYIMO*
Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu imelikataa ombi la
Mawakili wanaomtetea mtuhumiwa wa mauaji ya muigizaji wa filamu nchini Marehemu
STEVEN KANUMBA, ELIZABETH MICHAEL maarufu kwa jina la LULU la kutaka kesi hiyo
isikilizwe katika mahakama ya watoto kutokana na mtuhumiwa huyo kuwa na umri wa
chini ya miaka 18.
Akizungumza
mahakamani hapo Hakimu mfawidhi
AUGUSTINE MMBANDO
wa Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, amesema ELIZABETH anakabiliwa na kosa la
mauaji na mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji isipokuwa
mahakama Kuu na kuwataka kupeleka ombi hilo katika mahakama
hiyo.
Awali wakili wa Serikali katika kesi hiyo ELIZABETH
KAGANDA baada ya kupokea cheti cha kuzaliwa cha ELIZABETH amesema ipo haja yake
kufanyika kwa uchunguzi kuhusiana na umri wa mshitakiwa huyo kutokana na maelezo
aliyoandika polisi wakati alipokamatwa kuwa ana umri wa miaka 18 wakati cheti
hicho kinaonyesha ana umri wa miaka 17.
Wakili huyo pia amesema katika cheti hicho limeandikwa
jina la DIANA ELIZABETH wakati mtuhumiwa alitaja jina lake kuwa ni ELIZABETH
MICHAEL?? jambo ambalo mawakili wa upande wa utetezi, wamesema mara nyingi
wakristo huwa wanatumia majina mawili na kudai kuwa cheti hicho ni
halali.
Kesi hiyo itatajwa tena MAY 21, mwaka huu ambapo
uchunguzi bado haujakamilika.
hao watu wa tanzania ni wa ajabu sana, huyo mtoto ana kesi ya uuwaji na ushahidi mpaka sasa km kauwa hamna! kinachoonekana kuwa kanumba kafa kwa kuanguka kwa kishindo kikubwa ambacho anaweza kuwa alitetereka yee mwenyewe ktk kutaka kumuonyesha lulu kuwa yeye ni mwanamme (ktk kumtishia kumpiga). kwa kweli inasikitisha hasa pale huyo mtoto anatakiwa apewe haki yake, si muuwaji hata kidogo. huyo kanumba washajilia nyama kwao shinganya huko na saa hizi wanakatesa katoto ka watu tu!
ReplyDelete