Mwili wa marehemu Faustine Lyimo maarufu kwa jina la Mangi ukitolewa gesti.
Mwili wa Mangi ukiingizwa kwenye gari.
Gari lenye mwili wa Mangi likiondoka eneo la tukio.
Wananchi waliofika eneo la tukio.
Stori: Dunstan Shekidele, MorogoroDEREVA wa daladala anayepiga ‘ruti’ zake kati ya Mgeta, Matombo Mkuyuni na Morogoro Mjini, Faustine Lymo maarufu kwa jina la Mangi, mkazi wa Mtaa wa Msikitini mjini hapa amekutwa amekufa kwenye gesti iitwayo Flamingo.
Tukio hilo lilijiri hivi karibuni katika gesti hiyo iliyopo jirani na klabu ya pombe za kienyeji ya Manzese ambapo Mangi alikuwa amechukua chumba kabla ya kutoka kwenda chooni ulikokutwa mwili wake.
Tukio hilo lilithibitishwa na mwenyekiti wa Mtaa wa Msikitini, Ramadhan Kuka na Msemaji wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, Idd lbrahim huku kukiwa na maelezo kuwa Mangi alikuwa akisumbuliwa na kifua. Mwili wake ulisafirishwa kwenda kupumzishwa kijijini kwao, Vunjo mkoani Kilimanjaro.
Miss FB say: Ruwa Mangi akuambilyie necha"
RIP mangi"
ReplyDelete