Hapa wakiwa kwenye picha ya pamoja Missy Temeke atuonyesha Ubunifu wake .nguo hiyo alovaa "(Fab Dress) keep it up my dear so proud of you " |
Balozi wa Tanzania nchini
Marekani na Mexico Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar akiwasili kwenye ukumbi wa J.W
Marriot Mjini DC kuhudhuria dhifa ya chakula cha usiku kusherehekea siku ya
Africa tarehe 23 Mei 2012. Anayemuongoza Balozi ni flag bearer model wa
Kitanzania Hamisa au Miss Temeke ambaye alibuni vazi la kitanzania mahsusi kwa
shughuli hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa,Dkt Asha-Rose Migiro akihutubia kwenye hafla hiyo iliyofanyika kwenye
hoteli ya J.W Marriott jijini Washington DC Marekani "
Mhe. Balozi Maajar akifuatilia
salamu za Mhe. Kalonzo Musyoka, Makamu wa Rais wa Kenya alizotoa kwenye hafla
hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya J.W Marriott jijini Washington DC Marekani
"
Mkuu wa Utawala Ubalozini Mrs.
Lily Munanka akiwa na mgeni wa Tanzania kwenye hafla hiyo Rais wa gazeti la
Washington Times Bw. Thom McDevitt pamoja wakifuatilia salamu za Dkt Asha-Rose
Migiro alizotoa kwenye hafla hiyo"
Meza ya Tanzania ikiwa na
maafisa wa ubalozi wa Tanzania na wageni wao, Kulia ni Brg. General Maganga,
Mwambata Jeshi; Mr. Felix Ndunguru na Jesuit Temba, maafisa wawili kutoka Wizara
ya Maliasili na Utalii waliopo Washington DC kuhudhuria mikutano mbalimbali
kuhusu uhifadhi wa masalia ya binadamu wa kale yaliyovumbuliwa Tanzania.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa,Dkt Asha-Rose Migiro akiwa pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani
na Mexico Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar"
Snap za pamoja zikiendelea ,Wamependezaje na hata nyuso zao zasema yote shughuli zilifana sana" |
Snap time ,wacha snap zisema yote kwa Walimwengu" |
Maafisa wa ubalozi kwenye
picha za pamoja na Dkt Asha-Rose Migiro na Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar kwenye
hafla hiyo ya chakua cha usiku.
Hakuna kizungumzacho ukweli kama photo's" |
Mpaka chini watu wangu ,hapa Twaonyeshwa wasokuwepo tulokosa kushuhudia" |
Camera bado zafanya kazi yake " na haya ndiyo matokeo ya Upendo ,Amani na Umoja" |
No comments:
Post a Comment