KITENDA WILI"NYUMBA YANGU NDOGO LAKINI INAENEA WATU WENGI' MBUTA NANGA!!

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO BLOG

FLORA LYIMO BLOG

FLORA

FLORA

FLORA NA RAIS JK

FLORA NA RAIS JK

FLORA NA MH PINDA

FLORA NA MH PINDA

SHINY ,HEALTHY-LOOKING AND GORGEOUS HAIR' WHATSAPP +44 778 7471024

SHINY ,HEALTHY-LOOKING AND GORGEOUS HAIR' WHATSAPP +44 778 7471024

Sunday 15 April 2012

* IN YOU BEEN SNAP BLOG * WOSIA KUTOKA KWA MAMA MZAZI WA MAREHEMU STEVEN KANUMBA KWA SHIWATA!!


Marehemu Steven Kanumba"
 
Na Peter Mwenda"

MAMA Mzazi wa aliyekuwa msanii wa filamu nchini marehemu Steven Kanumba amewataka wasanii wanachama wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) kuendeleza ushirikiano alioacha mwanae.



Akizungumza katika ibada ya kumuombea mwanae iliyoandaliwa na (SHIWATA) leo Dar es Salaam, Mama Kanumba alisema amefarijika kuona wasanii wanaendelea kumuombea mwanae kila kona ya nchi.

"Nawashukuru SHIWATA kwa moyo wa upendo na ushirikiano mlionesha kwa familia yangu, naomba muendeleze ushirikiano mliokuwa nao wakati mwanangu akiwa nanyi, endeleeni kushirikiana" alisema Mama Kanumba.

Katika ibada hiyo iliyoongozwa na mchungaji wa Kanisa la Elim Pentekoste Ilala Bungoni, Mchungaji Livingstone Mwaitela alisema wasanii na familia ya Kanumba wasisononeke kwa sababu Mungu alimpenda
mtoto wao huyo zaidi.

Alisema wasanii waendelee kumkumbuka mwenzao kwa kubadili mambo yasiyompendeza Mungu badala yake wajiandae kwa kufanya mambo ambayo yanampendezesha na kujiweka tayari siku akiwaita wawe tayari.

Mwenyekiti wa SHIWATA,Caasim Taalib alisema Kanumba alikuwa mwanachama wao namba 648 akiwa mmoja wa waliojitokeza kutafuta eneo kwa ajili ya kujenga nyumba za wasanii kutoka Bagamoyo, Kisarawe na hatimaye kufanikiwa kupata eneo Mkuranga.

Marehemu Kanumba alifariki Aprili 5, wakati akikimbizwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya kuanguka nyumbani kwake Sinza kufuatia ugomvi wa mapenzi na msanii mwenzake Elizabeth Michael (Lulu).

No comments:

Post a Comment