Flaviana Matata akishindwa kujizuia na kuangua kilio
wakati wa ibaada ya kumbukumbu ya miaka 16 ya ajari ya meli ya MV Bukoba
alipotembelea baadhi ya makaburi ya watu waliopoteza maisha katika ajari hiyo
yaliyopo Igoma jijini Mwanza, katika ajali hiyo Flaviana alimpoteza pia mama
yake mzazi. Flaviana akionyesha moja ya maboya yenye nembo ya
foundation yake aliyokabidhi katika kumbukumbu ya miaka 16 ya ajali ya MV Bukoba
ikiwa ni kampeni yake ya kupunguza ajali za majini nchini
Tanzania.
Historia imewekwa leo na Flaviana Matata alipokabidhi
msaada wa maboya (life vests) 500 kwa Shirika la Meli la Taifa (Marine Services
Co Ltd) kama sehemu ya kumbukumbu ya MV Bukoba - ambapo ni miaka 16 tokea meli
hiyo ilizama na kuua watu takriban 1,000 akiwa pamoja na mama yake
Flaviana"
Flaviana Matata akiwasha
mshumaa pamoja na Jackie Sikawa ,Jema Kimbu na Maria Sarungi... kama sehemu ya
kumkumbuka ya mama yake mzazi ambaye alimpoteza katika ajali ya MV Bukoba miaka 16
iliyopita.... R.I.P mama Flaviana "Amen"
Flaviana Matata akiweka shada
kwenye kaburi lisiyo na jina Igoma jijini Mwanza kama sehemu ya kumbukumbu ya
watu waliopoteza maisha yao katika ajali ya MV Bukoba. Flaviana alimpoteza mama
yake mzazi.
No comments:
Post a Comment