KITENDA WILI"NYUMBA YANGU NDOGO LAKINI INAENEA WATU WENGI' MBUTA NANGA!!

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO BLOG

FLORA LYIMO BLOG

FLORA

FLORA

FLORA NA RAIS JK

FLORA NA RAIS JK

FLORA NA MH PINDA

FLORA NA MH PINDA

SHINY ,HEALTHY-LOOKING AND GORGEOUS HAIR' WHATSAPP +44 778 7471024

SHINY ,HEALTHY-LOOKING AND GORGEOUS HAIR' WHATSAPP +44 778 7471024

Monday 7 May 2012

*IN YOU BEEN SNAP BLOG* MAWAKILI WA LULU WAKATALIWA OMBI LAO LEO 07/5/2012 NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU".

*MKILETEWA HAPA NA MISS FB FLORA BAHATI LYIMO*


Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu imelikataa ombi la Mawakili wanaomtetea mtuhumiwa wa mauaji ya muigizaji wa filamu nchini Marehemu STEVEN KANUMBA, ELIZABETH MICHAEL maarufu kwa jina la LULU la kutaka kesi hiyo isikilizwe katika mahakama ya watoto kutokana na mtuhumiwa huyo kuwa na umri wa chini ya miaka 18.
Akizungumza mahakamani hapo Hakimu mfawidhi AUGUSTINE MMBANDO wa Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, amesema ELIZABETH anakabiliwa na kosa la mauaji na mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji isipokuwa mahakama Kuu na kuwataka kupeleka ombi hilo katika mahakama hiyo.
Awali wakili wa Serikali katika kesi hiyo ELIZABETH KAGANDA baada ya kupokea cheti cha kuzaliwa cha ELIZABETH amesema ipo haja yake kufanyika kwa uchunguzi kuhusiana na umri wa mshitakiwa huyo kutokana na maelezo aliyoandika polisi wakati alipokamatwa kuwa ana umri wa miaka 18 wakati cheti hicho kinaonyesha ana umri wa miaka 17.
Wakili huyo pia amesema katika cheti hicho limeandikwa jina la DIANA ELIZABETH wakati mtuhumiwa alitaja jina lake kuwa ni ELIZABETH MICHAEL?? jambo ambalo mawakili wa upande wa utetezi, wamesema mara nyingi wakristo huwa wanatumia majina mawili na kudai kuwa cheti hicho ni halali.

Kesi hiyo itatajwa tena MAY 21, mwaka huu ambapo uchunguzi bado haujakamilika.
 

1 comment:

  1. hao watu wa tanzania ni wa ajabu sana, huyo mtoto ana kesi ya uuwaji na ushahidi mpaka sasa km kauwa hamna! kinachoonekana kuwa kanumba kafa kwa kuanguka kwa kishindo kikubwa ambacho anaweza kuwa alitetereka yee mwenyewe ktk kutaka kumuonyesha lulu kuwa yeye ni mwanamme (ktk kumtishia kumpiga). kwa kweli inasikitisha hasa pale huyo mtoto anatakiwa apewe haki yake, si muuwaji hata kidogo. huyo kanumba washajilia nyama kwao shinganya huko na saa hizi wanakatesa katoto ka watu tu!

    ReplyDelete