KITENDA WILI"NYUMBA YANGU NDOGO LAKINI INAENEA WATU WENGI' MBUTA NANGA!!

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO BLOG

FLORA LYIMO BLOG

FLORA

FLORA

FLORA NA RAIS JK

FLORA NA RAIS JK

FLORA NA MH PINDA

FLORA NA MH PINDA

SHINY ,HEALTHY-LOOKING AND GORGEOUS HAIR' WHATSAPP +44 778 7471024

SHINY ,HEALTHY-LOOKING AND GORGEOUS HAIR' WHATSAPP +44 778 7471024

Thursday 1 January 2015

WHATS NOW'' KAMA HILI GAZETI LA MWANANCHI LILIKUPITA SASA UNAWEZA KULIPATA HAPA NA KUMSOMA FLORA LYIMO NDANI YA ''MAISHA'' KWENYE HILI THE TOP TANZANIAN NEWS PAPER'



THE PROUD TANZANIAN MISS FLORA LYIMO '' KWA UFUPI ..IKIWA WAIPENDA NCHI YAKO'' ISHI UKIJIVUNIA KUWA MWANANCHI WAKE NA KUFANYA MOJA AU MENGI KUISHIKILIA ILI ISIANGUKE WALA KUCHAFULIWA KWA AINA YOYOTE'' HASA KUIJENGA'' NCHI HUJEJWA NA WANACHI WENYEWE''SO NAJIVUNIA TANZANIA NA NITAITANGAZA POPOTE PALE NILIPO HADI KIFO '' RUWA MANGI''

Kutoka ‘hausigeli’ mpaka kumiliki maduka (3)
Wiki iliyopita Flora Lyimo au Mbuta Nanga anayeishi na kufanya biashara za maduka
ya nguo katika mitaa ya Oxford inayosifika kwa kuwa na wabunifu wakubwa duniani,jijini London nchini Uingereza,alisimulia mkasa wa maisha yake ya kutafuta mafanikio.
Na Herieth Makwetta, Mwananchi
Licha ya kuelezea safari yake iliyoanzia Tarafa ya Kilema, Wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro mwaka 1989, kazi za ndani, uchezaji chakacha na hatimaye kufika jijini London, alielezea uzoefu wake katika kuuza maduka ya watu na kukusanya mtaji uliomwezesha kufungua biashara yake ya duka la nguo. Endelea…Mbuta Nanga anasema baada ya kufanikiwa kupata duka la kwanza, alijitahidi kuhamasisha wateja na hatimaye mwezi huu wa Desemba anatarajia kufungua duka lake la
pili.“Mwezi huu nafungua duka lingine mtaa unaoitwa Posh (Charing Cross ). Ni duka ambalo
litakuwa na mavazi ya kinamama na mabegi pamoja na vitu vya urembo zaidi, yaani mimi kwa kweli napenda kufungua maduka yangu niweze kuwauzia watu vile vitu ambavyo mimi mwenyewe
nilikuwa navihitaji madukani na navikosa,” anasema.
Anasema dukani kwake yanapatikana mabegi mazuri kwa bei poa, kwani ameamua kufanya hivyo
baada ya maduka mengi kuuza bidhaa hizo kwa bei ghali.“Nipeni miaka miwili tu mtaamini kwamba kweli naweza, biashara yangu nilianza rasmi mwaka 2013,ila nilikuwa pia nafanya biashara

Flora akiwakwenye dukalake katikamitaa ya Oxfordjijini London.
MAISHA
za kuwatumia kinadada hasa mabegi kwa njia ya mkopo ‘express’, ambao nilikuwa nawapa mabegi kumi kumi nawapa bei zangu ambazo watanirudishia baada ya kumaliza kuyauza hayo mabegi kumi,”anasema.Mbuta Nanga anasimulia kwamba wahusika hao alikuwa anawapa masharti
kwamba atakayemaliza mapema basi alimtumia mengine.“Ila baada ya kuja kupata duka na
kuanza kulishughulikia kwa ubize uliokuwepo dukani hapo nikaamua kusimamisha kwanza zoezi hilo, ila hiyo biashara bado ipo na bado nina watu zaidi ya 60 huko Tanzania, mikoa michache ambayo wanauza bidhaa zangu wanajipatia hela zao na mimi najipatia zangu,” anasema
na kuongeza: “Hiyo ndiyo njia moja ambayo naona naweza kuwasaidia kinamama wenzangu,
hasa wasichana wadogo ambao wengi wao ndiyo hao ninaowaona kwenye magazeti wanashikwa kwa kosa la kujiuza barabarani na hii ni kukosa nafasi za kazi.”Mbuta Nanga anasema kama angekuwa
na uwezo zaidi, angependa kuwapa mikopo hiyo ya bidhaa wauze kwa wingi ili waweze kujiondoa kwenye hiyo biashara ya kujiuza na kwamba mkopo wa biashara aliousitisha utarudi tena.
“Ikiwa kuna wateja wanahitaji bidhaa zangu, watakuwa wanapata kwa ‘kuoda’ au kwa mimi kuwaambia wauzaji wa‘Flora Lyimo mkopo express’ wapo wapi, ila kwa sasa hivi kwa kuwa nipo bize na haya maduka nilisimamisha, lakini pia vilevile nina mpango wa kufungua maduka Tanzania, ikiwa nimeanza hapa UK nitamalizia huko,” anasema. Kutapeliwa Anasema awali alifikiria kuwekeza nyumbani, lakini wenye tamaa ya fedha wakakatisha ndoto zake. Lakini sasa
ameamua kwamba kabla ya kuwa na duka la nguo, ana mpango pia wa kufungua
mgahawa na baa.“Kabla ya duka la nguo nataka kufungua baa na ‘restaurant Buffet, maana
naona maduka ya nguo na mabegi ni mengi sana kila sehemu Tanzania.”“Ninapenda sana kula na ninapokuja Tanzania sijapata mahali penye chakula kizuri, kwa hiyo nina ndoto yangu nyingine, ila sijui kama kuna uwezekano huo maana huko kusema ukweli sikufahamu vizuri kama ninavyofahamu Uingereza, tuseme Moshi naifahamu vizuri hasa vijijini kwa kuwa ndipo nilipokulia kwa miaka 15, hivyo naona nitachukua muda kuhakikisha nafanya kazi na watu wasio matapeli,” anasema. Mbuta Nanga anasema ameshatapeliwa na wanaume wengi kutoka hapa nchini. “Nilijaribu kuwekeza nyumbani, lakini kwa bahati mbaya kuwa wanaume wamenitapeli sana hasa kwa kutumia njia ya mapenzi, kujifanya wana mapenzi na mimi tufanye biashara fulani niwatumie bidhaa na pesa halafu wakaishia mtini, ila sitowataja hapa na pia nimeshamwachia Mungu, wajue pia vitu vya utapeli au
wizi havidumu,” anasema Flora. Uwekezaji Tanzania Hata hivyo, Mbuta Nanga anasema
sasa hivi anachowekeza Tanzania ni pesa zake katika benki mbalimbali.“Yaani hapa UK siaminigi kuacha pesa zangu benki huwa naona bora nyumbani ili na ndugu zangu waweze kuzitumia kwa urahisi ikiwa kumetokea dharura, kwani naona kama kizungu kitawasumbua kwa hiyo pesa zangu zikiingia UK nazituma nyumbani, na kama nilivyosema nina mpango wa kufungua baa na
mgahawa, watu wawe wanakula bila kipimo na kwa uwezo wa matumbo yao hahahaaa,” anacheka.
Akiwazungumzia wanawake ambao hawajishughulishi, Mbuta Nanga anasema ni wakati wao kuamka sasa.“Wakati ndiyo huu amka sasa, fikiria ni nini haswa unaweza kukifanya na anza
kuomba Mungu na huku ukikitafuta, mwisho wa siku utakipata na utashangaa wewe mwenyewe, kinamama msiogope kupoteza hela, ukiwa una kipesa chako mahali wewe kitafutie biashara, anza
kidogo kidogo na usianze kwa kuuza vitu kwa bei ghali ukifikiria ndiyo utatajirika haraka, uza kwa kupata faida ndogo ndipo utapata faida kubwa hapo baadaye,”
anasema. Ikiwa Mbuta Nanga ni mtu anayeishi nje ya nchi ambako teknolojia imekua,
anasema mitandao ya kijamii anaiogopa kwa sasa, kwani Watanzania wengi wamekuwa wakiitumia vibaya badala ya kuitumia katika kutangazia biashara zao.“Mitandao ya kijamii nayoona inafaa
kwa kunitangazia biashara zangu ni Facebook na Blogu yangu yaani Instagram kule ni jumba la dhambi kwa Watanzania, kule nilikuwepo kwa miezi mitano na nilikuwa naitumia kwa kila kitu ila nilipokuwa naweka vitu vyangu vya biashara hamna mtu aliyekuwa ananifolo au kuniambia
hata vipi nipateje? “Yaani walikuwa wachache sana na pia siyo kwamba wanataka kweli wanauliza
tu, lakini nikiweka umbea yaani nagombana na mtu au niweke picha mbaya utaona watakavyoitana na kuanza kunifuata kama nyuki, nilitoka huko na nikasema sirudi tena kule hata kwa fimbo,” anasema Mbuta Nanga.Kuhusu familia, ndoa Mbuta Nanga ambaye ni mcheshi na
mkarimu, anasema mpaka sasa bado hajabahatika kuwa na familia.“Sina mtoto na sijawahi kuolewa
harusi ya kuvaa gauni jeupe kanisani, hiyo ni ndoto yangu nyingine ninayoisubiria.Nasubiri kupata mume mzuri atakayenipenda kwa mapenzi ya dhati,awe mrefu na mwenye sauti nzuri na mchapakazi, yaani awe na vitu viwili nilivyoviandika katika kitabu changu cha kumbukumbu. Ila watoto maajaliwa, sijawahi kukaa chini nikiomba niwapate,niko bize kuyaweka maisha yangu sawa
kwanza,” anasema''

No comments:

Post a Comment