*MKILETEWA HAPA NA MISS FB *Huku nikiwatakieni MAANDALIZI MEMA YA 50YRS YA UHURU WETU WATANZANIA"
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
katika salamu zake za mwaka mpya wa 2011 kwa
Watanzania tarehe 31 Desemba, 2010 kati ya masuala mbalimbalialiyozungumzia ni pamoja na kuliarifu Taifa kuhusu Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Aidha, Mhe. Rais aliiagiza Serikali kuhakikisha kuwa maadhimisho hayo yanafanyika kwa uzito
(i.) Kuutangaza mwaka 2011 kuwa ni mwaka wa maadhimisho ya
miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambapo kutafanyika
sherehe kubwa na ya aina yake nchi nzima na kilele chake
kuwa tarehe 9 Desemba, 2011,
(ii.) Kila Wizara, Idara na Taasisi za Serikali na Sekta binafsi ifanye
tathmini ya kina ya mafanikio yake na kuandika katika kitabu ili
kuhifadhi kumbukumbu hizo muhimu kwetu na vizazi vijavyo,
(iii) Yafanyike maonesho maalum katika Uwanja wa Maonesho wa
Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kote mikoani kwenye
Viwanja vya Maonesho kuelezea mafanikio yaliyopatikana
katika nyanja mbalimbali katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru
wa Tanzania Bara, na
(iv) Kuanzisha mchakato wa kutazama upya Katiba ya Nchi yetu
kwa lengo la kuihuisha ili hatimaye tuwe na Katiba
inayoendana na Taifa lenye umri wa nusu karne.
(1.2) Kufuatia agizo hilo la Rais, Serikali imeandaa Mwongozo
utakaotumiwa na Wizara, Mikoa na Taasisi katika kuadhimisha
Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.




No comments:
Post a Comment