Diamond ! |
Pichani hapa huku akicheka bila kufaham chakumfanye acheke ..ni mwaandishi wa habari Francis Godwin akiwa amelivaa koti lake lililochanwa ! |
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya,Diamond akiwa amewekwa chini ya ulinzi wa mashabiki uwanjani hapo ambako alikuja tolewa na polisi.Diamond akisimamiwa kuimba bila ya vyombo vya muziki jukwaani Iringa.Diamond akiwa chini ya ulinzi wa polisi akitolewa Hotelini na kuelekea kituoni.Mwandishi wa Habari wa Mkoani Iringa,Francis Godwin akiwa amechaniwa vibaya koti lake na Diamond mara baada ya kumvaa na kumpiga.
Na Mwandishi Wetu,Iringa.
MSANII maarufu wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul a.k.a Diamond na wacheza show wake wawili wamejikuta wakifunga mwaka vibaya baada ya kutupwa rumande kwa kosa la kumshambulia na kuharibu mali za mwandishi wa habari wa mkoani Iringa Francis Godwin.
Sakata la Diamond kumshambulia mwanahabari huyo maarufu hapa nchini lilitokana na hatua ya utata uliokuwa umejitokeza katika uwanja wa Samora mjini Iringa ambako Diamond alipaswa kufanya onyesho lake ya kuuanga na kuukaribisha mwaka 2012 .
Hata hivyo onyesho hilo lilionyesa kuwa na kila aina ya utapeli baada ya ratiba kuonyesha kuanza saa 8 mchana na kumalizika mida ya saa 12 za jioni na baada ya hapo uwanja huo ulipaswa kutumiwa na umoja wa Makanisa mkoani Iringa kwa ajili ya mkesha wa kufunga mwaka na mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christina Ishengoma ndie alikuwa mgeni rasimi.
Hivyo kutokana na msanii huyo kushindwa kuonekana hadi mida ya saa 11.50 jioni mashabiki kiduchu ambao walikuwa wameingia katika uwanja huo walilazimika kumvaa mmoja kati ya wahusika katika onyesho hilo ambaye alikuwa akichukua fedha za kiingilio mlangoni na kuanza kuhoji sababu ya onyesho hilo kukwama na msanii Diamond na Afande Sele ambao walipaswa kupagawisha kutoonekana hadi mida hiyo na kuhoji sababu ya tiketi za chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) ambazo zinaonyesha kuna mchezo wa kirafiki kati ya Asante Kotoko ya Ghana na Marafiki wa Uhuru mchezo uliochezwa 12/11/2011 uwanja wa Taifa na kiingilia ni shilingi 5000 huku wao wamefika kuona wasanii na sio mechi.
Hata hivyo haikuchukua muda ghafla Costa ambayo ilikuwa imembeba Diamond na wacheza show wake bila Afande Sele iliwasili uwanjani hapo na kufanya mashabiki kupunguza jazba.
Kutokana na hali ya utulivu kurejea uwanjani hapo mwandishi wa habari huyo ambaye ni mmiliki wa blogu ya www.francisgodwin.blogspot.com na makampuni ya New Habari LTD alimfuata na kwa nia ya kutaka kufanya nae mahojiano na kujua sababu za kuchelewa katika show hiyo hapo ndipo Diamond alipogeuka mbogo na kupokonya kamera ya kuirusha chini baada ya kufuta picha .
Baada ya hapo mashabiki walimlazimisha Diamond kupanda jukwaani kuimba vinginevyo wangemchapa hivyo kulazimika kupanda jukwaani huku akisimamiwa kwa bakora na mawe ,pamoja na kupanda jukwaani bado alishindwa kuimba baada ya wale waliokodisha vifaa vya muziki kugoma kupiga muziki kwa madai muda wao umekwisha huku watu wa mkesha wa makanisa nao wakipinga jukwaa la ibada ya mkesha kutumika kwa mambo ya kidunia hali iliyozua utata .
Hali hiyo ilimfanya Diamond kuchanganyikiwa zaidi na kushindwa kushuka jukwaani kwa kuhofia kichapo toka kwa mashabiki kutokana na hali hiyo mwandishi alianza kufanya mahojiano na kuchukua picha za mashabiki kusubiri na kumsimamia msanii huyo kabla ya kuruka jukwaani na kikosi chake na kuanza kumchapa mwandishi huyo ambaye pia alionyesha kukabiliana nao kwa kiasi na kusaidiwa na mashabiki .
Kutokana na tukio hilo mwandishi huyo wa habari Godwin alipoteza camera yake yenye thamani ya shilingi milioni 1.5, simu moja yenye thamani ya shilingi 300,000 huku Laptop yake ndogo aina ya Acer ikiharibiwa na msanii huyo.
Tukio hilo lilifikishwa polisi na Diamond kufunguliwa mashtaka ya kushambulia kwa RB namba IR/RB/ 7700/2011 na baada ya muda mida ya saa 1.30 usiku jeshi la polisi lilikwenda kumkamata msanii huyo na vijana wake wawili ambao walikuwa katika Hotel ya Staff Inn Anex mjini hapa wakijipumzisha na kupelekwa mahabusu hadi asubuhi .
Mratibu wa show hiyo Mike T akiomba msamaha kwa mwandishi huyo alisema kuwa msafara wa Diamond ulikuwa ukitokea Mbeya katika uwanja wa Sokoine ambako pia Show ilikwama kutokana na mvua kubwa kunyesha na baada ya hapo walianza safari kwa ajili ya kuja Iringa na kukwama kufika kwa wakati kutokana na basi lao la kwanza kuharibika na kulazimika kukodi Costa na kufika kwa mida mibaya Iringa na kuwa baada ya Iringa Msafara huo ulitaraji kwenda jijini Dar es Salaam kuzindua Albam yake .
No comments:
Post a Comment