KITENDA WILI"NYUMBA YANGU NDOGO LAKINI INAENEA WATU WENGI' MBUTA NANGA!!

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO BLOG

FLORA LYIMO BLOG

FLORA

FLORA

FLORA NA RAIS JK

FLORA NA RAIS JK

FLORA NA MH PINDA

FLORA NA MH PINDA

SHINY ,HEALTHY-LOOKING AND GORGEOUS HAIR' WHATSAPP +44 778 7471024

SHINY ,HEALTHY-LOOKING AND GORGEOUS HAIR' WHATSAPP +44 778 7471024

Sunday 18 August 2013

BY :FLORA LYIMO~ KIT*MBI T*MBI AFIA GESTI AKIWA NA MKE WA MTU'' MBUTA NANGA!!!!!!!!!!!!!

      
 


Stori:Gladness Mallya na Haruni Sanchawa
TUKIO la aibu limetokea Kiwalani jijini Dar Siku ya Idd Pili pale mume wa mtu, Hamad Kipondo (46) alipofariki dunia ndani ya nyumba ya wageni ‘gesti’ akidaiwa kuwa na mke wa mtu ambaye ni mpangaji mwenzake.
Mke wa marehemu akisaidiwa kutolewa eneo la tukio
Kwa mujibu wa mtoa habari wetu (jina tunalo), Kipondo na mwanamke huyo, Latifa Suleiman (25), ni wakazi wa Kigogo, Dar ambao walifika   katika gesti hiyo kwa ajili ya kusaliti ndoa zao.

LATIFA NI MKE WA MTU
Sosi huyo alithibitisha kuwa Latifa ni mke wa mtu na siku ya tukio mumewe alikuwa safarini hivyo wawili hao wakatumia nafasi hiyo kwenda kufurahisha nafsi zao.
Polisi wakiingiza mwiliwa marehemu kwenye gari
MUME AMDANGANYA MKEWE
Ilidaiwa kuwa kabla ya kuondoka nyumbani kwake, Kipondo alimdanganya mkewe, Salma Abdallah kuwa anakwenda kwenye mihangaiko ya kutafuta fedha.MOYONI ALIJUA NI UONGO
Ilisemekana kuwa mke alikubali maneno ya mumewe lakini mwanaume huyo moyoni mwake alijua kabisa kwamba anamdanganya mkewe kwani wakati huo alikuwa ameshapanga kukutana na Latifa huko Kiwalani katika gesti hiyo (jina  tunaliminya).Majilani wakishudia tukio hilo'
PICHA KAMILI Habari kamili zilisema kuwa baada ya mwanaume huyo kuondoka nyumbani, mke aliendelea na shughuli zake kama kawaida huku akiwa hana wasiwasi wowote wa kusalitiwa na mumewe.
SIMU YA KIFO Ilipotimu saa 8:00 mchana, mke alipokea simu kutoka kwa mtu asiyemfahamu akimwaambia kuwa mumewe Kipondo amepatwa na matatizo, hivyo anatakiwa kufika haraka Kiwalani.
Mke akiwa hajui kama amepigiwa simu ya kifo, alitafuta usafiri wa haraka wa kuweza kumfikisha Kiwalani ili kujua kile kilichomsibu mumewe.
Njiani alikuwa akitembea huku akiwa na wasiwasi na wakati mwingine aliongea peke yake akiomba Mungu amwepushie balaa mumewe.
MSHTUKO Mke alipofika eneo la tukio, kwanza alipatwa na mshtuko kwa kuliona gari la polisi aina ya Land Rover 110 ‘difenda’ na watu wakiwa wamejazana.
Moja kwa moja alihisi mumewe alikuwa amekamatwa na polisi, wasiwasi ukaongezeka huku akijiuliza maswali lukuki kwamba kitu gani mumewe atakuwa amekifanya hadi kushikiliwa na askari wale.
VILIO VYAMSHTUA Kikubwa kilichomshtua mke huyo ni pale alipowaona baadhi ya watu anaowafahamu wakiangua vilio.
Hisia za machozi zikaanza kumvaa bila kujua hasa kilichompata mumewe.
APASULIWA BOMU
Baadhi ya ndugu waliokuwa wakiangua vilio kwa uchungu na kulitaja jina la mumewe, walipoona mke hajapata picha kamili wakaamua kumpasulia bomu kwa kumwambia kilichojiri.
KILIO Baada ya kuambiwa kilichotokea, mke huyo akaanza kulia kwa uchungu kuliko mtu mwingine.
Kilio chake kilikuwa na sababu kubwa mbili; kwanza ni kifo cha mumewe, pili usaliti aliofanyiwa.
MBAYA ZAIDI“Mbaya zaidi marehemu alikuwa na mke wa mpangaji mwenzake na ilikuwa ni Siku ya Idd Pili.
“Kilio kiliongezeka maradufu kwa kuwa alikuwa akimwamini  na kushirikiana na mpangaji huyo mwenzake kwa njia moja au nyingine, akijenga uaminifu mkubwa kwamba hawezi kumsaliti,” alisema sosi wetu.
MUME MOCHWARI, MKE WA MTU RUMANDE Hatimaye polisi waliuchukua mwili wa marehemu Kipondo na kuuingiza kwenye gari kwa ajili ya kuupeleka Hospitali ya Amana kuuhifadhi.
Kwa upande wake Latifa alichukuliwa na kupelekwa katika Kituo cha Polisi cha Buguruni, Dar.
CHANZO CHA KIFO Mpaka habari hii inaandikwa ukweli anao Latifa tu ambaye ndiye anayeweza kusimulia kilichotokea hadi kukatisha uhai wa Kipondo hivyo tunaendelea kufuatilia.
Marehemu Kipondo amezikwa Jumatatu iliyopita katika Makaburi ya  Chang’ombe, Temeke, Dar na ameacha mjane na watoto wawili.

TUMESHIRIKI NA KUCHAMBUA KUTOKA GP''

No comments:

Post a Comment