KITENDA WILI"NYUMBA YANGU NDOGO LAKINI INAENEA WATU WENGI' MBUTA NANGA!!

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO BLOG

FLORA LYIMO BLOG

FLORA

FLORA

FLORA NA RAIS JK

FLORA NA RAIS JK

FLORA NA MH PINDA

FLORA NA MH PINDA

SHINY ,HEALTHY-LOOKING AND GORGEOUS HAIR' WHATSAPP +44 778 7471024

SHINY ,HEALTHY-LOOKING AND GORGEOUS HAIR' WHATSAPP +44 778 7471024

Wednesday, 11 December 2013

BY:FLORA LYIMO ~HAPPY 11/12/13 MY DEARS'' WATANZANIA MMEJIANDAA VIPI KUMKARIBISHA MALKIA WA HOLANZI MHE MAXIMA AMBAE ATAWASILI NCHINI TANZANIA LEO ''

MALKIA WETU NDIYO HUYO ''MHE.MAXIMA''

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Malkia wa Uholanzi Mhe. Maxima anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 11 Desemba, 2013 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu. 

Mhe. Maxima ambaye pia ni Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Mfumo Jumuishi wa Fedha katika Maendeleo atapokelewa na mwenyeji wake, Mke wa Rais, Mhe. Mama Salma Kikwete kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Baada ya kuwasili, Mhe. Maxima atafanya mazungumzo rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam pamoja na kushiriki katika Dhifa ya Kitaifa.

Aidha, tarehe 12 Desemba 2013, Malkia Maxima atafanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Mhandisi Christopher Chiza, Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Saada M. Salim na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Benno Ndulu. 

Siku hiyo hiyo Mhe. Maxima atazindua rasmi Mfumo Jumuishi wa Fedha wa Taifa katika hafla itakayofanyika Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Mfumo huo unalenga kuwanufaisha Wanawake na Vijana, hususan katika kuchangia usalama wa chakula, kilimo na maendeleo Vijijini.

Mhe.  Maxima ataondoka Dar es Salaam tarehe 13 Desemba, 2013 kuelekea Dodoma ambako ataendelea na ziara yake kwa kutembelea mashamba ya zabibu katika Kijiji cha Gawaye pamoja na kuzungumza na Wakulima. Mashamba hayo yanasimamiwa kwa ushirikiano kati ya Shirika la Chakula Duniani (WFP), Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD).  

Mhe. Maxima anatarajiwa kuondoka nchini siku hiyo hiyo jioni kurejea Uholanzi.

IMETOLEWA NA: 

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, 
DAR ES SALAAM. 
10 DESEMBA, 2013

No comments:

Post a Comment