KITENDA WILI"NYUMBA YANGU NDOGO LAKINI INAENEA WATU WENGI' MBUTA NANGA!!

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO BLOG

FLORA LYIMO BLOG

FLORA

FLORA

FLORA NA RAIS JK

FLORA NA RAIS JK

FLORA NA MH PINDA

FLORA NA MH PINDA

SHINY ,HEALTHY-LOOKING AND GORGEOUS HAIR' WHATSAPP +44 778 7471024

SHINY ,HEALTHY-LOOKING AND GORGEOUS HAIR' WHATSAPP +44 778 7471024

Monday 26 May 2014

BY FLORA LYIMO ~ MBUTA NANGA!! KITOMBI TOMBI APATIKANA MKE WA NDOA KAIOZESHA ARUSI YAKE NA MBUNGE ILIYOKUWA IZIYEYUSHE MIL'S 96 TZSH'' POLICE TANZANIA NAOMBA MUMKAMATE HUYU CHARLES NA APEWE KIFUNGO GELA MIAKA SABA..KUDADADEKI 'NA HICHO KIWE KIFUNGO CHA VITOMBI TOMBI WOTE WATAKAO WATAPELI WANAWAKE KWA NJIA YA MAPENZI''

Vicky Kamata ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya UVCCM, Mkoa wa Geita alikuwa afunge ndoa na mwanaume aliyejulikana kwa jina la Charles wa jijini…
Stori: WAANDISHI WETU
Hadi gazeti hili linaondoka kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi, Sinza jijini Dar juzi saa 10:00 jioni, ndoa ya Mbunge Vicky Kamata iliyokuwa ifungwe hapo iliyeyuka.
Vicky Kamata akiwa na Charles walipokuwa matembezini nchini China.
Vicky Kamata ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya UVCCM, Mkoa wa Geita alikuwa afunge ndoa na mwanaume aliyejulikana kwa jina la Charles wa jijini Dar.
KATEKISTA AZUNGUMZA NA IJUMAA WIKIENDA
Baada ya kuona muda unakwenda bila kuwepo kwa dalili za wahusika kufika  kufunga ndoa hiyo ambayo harusi yake ilidaiwa ingetumia shilingi milioni 96, wanahabari wetu walimtafuta Baba Paroko, Cuthbert Maganga ili kumsikia anasema nini kuhusu hilo.
Hata hivyo, mtu aliyedai ni katekista wa kanisa hilo alisema paroko alikwenda hija, Buguruni, Dar.
Kuhusu ndoa ya Vicky Kamata, katekista huyo alidai Jumapili ya Mei 18, 2014 ndani ya ibada za kanisa hilo ilitangazwa hadharani ‘laivu’ kwamba haitafungwa.
Vicky Kamata akiwa amelazwa baada ya kuugua ghafla katika Hospitali ya Tabata General jijini Dar.
SABABU ZA KANISA
Habari za ndani zilidai kuwa kanisa lilibaini upungufu mkubwa kwa bibi harusi na kumwambia ndoa haitakuwepo.
Upungufu huo ni pamoja na Vicky Kamata kushindwa kuwasilisha cheti chake cha ubatizo, pia hakuwahi kupata kipaimara. Ilidaiwa kuwa vitu hivyo kwa uchache wake ni kikwazo kikubwa kwa mtu kufikia daraja la Sakramenti ya Ndoa.
SABABU ZA NDANI
Ukiachana na sababu hizo za kanisa, Ijumaa Wikienda lilichimbua na kubaini sababu kuu 3 ambazo zilikuwa kisiki cha kufungwa kwa ndoa hiyo.
Vicky na Charles wakila bata.
SABABU YA KWANZA
Kwa mujibu wa chanzo, mwanaume aliyetaka kufunga ndoa na Vicky ana ndoa nyingine ya kanisa na imejaliwa kupata watoto kadhaa hivyo isingekuwa rahisi kufungwa kwa ndoa nyingine kwa mujibu wa maandiko ya Biblia. Mume mmoja mke mmoja mpaka kifo kiwatenganishe.
MKE ATINGA BUNGENI
Chanzo kilizidi kudai kuwa wiki iliyopita, mwanamke huyo ambaye jina halikupatikana, alitinga bungeni na kuonana na Spika wa Bunge, Anne Makinda ambapo alijitambulisha ndiye mke wa Charles anayetaka kufunga  ndoa na Vicky Kamata.
“Mke wa bwana harusi alikuja Dodoma juzi, akasaidiwa kuonana na spika na mbunge mmoja (jina tunalo).
“Alimwambia spika yeye ndiye mke wa ndoa wa Charles, ila walitengana. Lakini alisema pamoja na kutengana huko, ndoa ya Kikristo haifungwi mara mbili labda mmoja afe. Kwa hiyo mumewe hawezi kufunga ndoa na Vicky,” kilisema chanzo.
SABABU YA PILI
Sababu ya pili ilielezwa kuwa, Vicky asingeweza kufunga ndoa hiyo kwani mwanaume huyo alishatoa mahari kwa msichana mmoja (jina tunalo) wa jijini Dar na ukweni anajulikana.
“Alishatoa mahari kwa msichana mwingine mbali na Vicky, ukweni anajulikana.
Vicky Kamata akiwa katika pozi na mwanaume aliyepanga kuoana naye anayejulikana kwa jina la Charles wa jijini Dar.
“Sasa ilipotoka ile picha yake kwa mara ya kwanza kwenye Gezeti la Ijumaa (Mei 16, 2014) yenye kichwa cha habari ndoa ya Vicky itatumia shilingi milioni 96 ikawa kasheshe kwa yule msichana na ukweni, ndiyo jamaa akaamua kutangaza kubatilisha ndoa na Vicky,” kilisema chanzo.
SABABU YA TATU
Sababu ya tatu ilitajwa ni kitendo cha kuumwa. Wikiendi iliyopita, Vicky aliugua ghafla na kulazwa katika Hospitali ya Tabata General jijini Dar kwa hiyo isingekuwa rahisi ndoa kufungwa Jumamosi kutokana na hali yake kuwa mbaya.
WAANDISHI WATINGA HISPITALI
Ijumaa iliyopita, waandishi wetu walitinga kwenye hospitali hiyo na kukutana na daktari mmoja ambaye alikiri Vicky kulazwa hapo lakini alikataa waandishi wasimuone kwa sababu hayuko katika hali nzuri kiafya. “Ni kweli Vicky kalazwa hapa lakini hamuwezi kumwona, hayuko katika hali nzuri, anahitaji kupumzika jamani, please,” alisema daktari huyo.
HATIHATI ILISHAKUWEPO
Katika Gazeti la Uwazi la Mei 20, 2014 ukurasa wa mbele kulikuwa na habari ndogo yenye kichwa kisemacho; NDOA YA MIL. 96 YA VICKY KAMATA HATIHATI KUFUNGWA.
Katika habari hiyo ilielezwa kuwa ndoa  hiyo isingefungwa kutokana na kuibuka kwa mizengwe kibao.
Habari za ndani zilisema mizengwe hiyo iliibuka katika hatua za mwisho na kusababisha mwanaume kuamua kubatilisha ndoa hiyo ambayo ilikuwa ifungwe Mei 24, mwaka huu jijini Dar.
KIONGOZI MKUBWA SERIKALINI
Ilidaiwa kuwa baada ya kuibuka kwa zengwe na mume kutangaza ndoa basi, Vicky aliumia na kuzifikisha habari hizo kwa Spika Makinda ambapo naye alizifikisha kwa kiongozi mmoja mkubwa serikalini, hasa bungeni.
Kiongozi huyo alichukua jukumu la kumvutia waya bwana harusi na kumsihi kutochukua mawazo hayo na ikibidi ndoa ifungwe lakini mwanaume huyo alikataa katakata akisema mambo hayo ni ya kifamilia zaidi kwa hiyo yaachwe kwenye familia.
MAMA SITTA ASIKITIKA
Habari zinazidi kusema kuwa kati ya watu ambao wamehuzunishwa na kutofungwa kwa ndoa hiyo ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM), mheshimiwa Margaret Simwanza Sitta ambaye aliposikia kuyeyuka kwa ndoa hiyo alisikitika si kwa sababu alikuwa kwenye vikao vya harusi, bali pia aliuona wakati mgumu atakaoupata Mhe. Vicky.
WABUNGE WAULIZIA MICHANGO YAO
Pamoja na yote yaliyojitokeza, habari zinadai kwamba baadhi ya wabunge waliochanga pesa ili kufanikisha harusi hiyo tangu juzi wameanza kuulizia michango yao wataipataje kwa vile harusi basi tena!
“Huku Dom (Dodoma) hakukaliki bwana. Baadhi ya wabunge wameanza kuulizia michango yao, wanasema kama harusi haipo basi na chao wakipate,” alisema mbunge mmoja akiomba kuhifadhiwa jina.
WABUNGE WATAJWA KUINJINIA
Mbunge huyo alikwenda mbali zaidi kwa kusema kuwa kuna wabunge wametajwa ‘kuinjia’ zengwe la kutokufungwa kwa ndoa hiyo kwa sababu wanazozijua wao ambazo Ijumaa Wikienda haikupewa lakini inaendelea kuzichimba.
VICKY KAMATA
Vicky alipotafuwa kwa njia ya simu Jumamosi iliyopita ili azungumze lolote kuhusu kuyeyuka kwa ndoa yake hakupatikana hewani.

Imeandaliwa na Chande Abdallah, Nyemo Chilongani na Mayasa Mariwata.

No comments:

Post a Comment