
Utafiti mpya uliofanywa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii umeonyesha kuwa kutoboka kwa kibofu cha mkojo, kushamiri kwa kansa ya shingo ya uzazi, utasa na matatizo ya kisaikolojia kwa wanawake kunatokana na kasi kubwa ya utoaji mimba nchini. Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Mtumwa Mwako(pichani), akizungumza mjini hapa jana, alisema ripoti ya utafiti huo inaonyesha kwamba, utoaji mimba ndiyo chanzo kikuu cha matatizo mengi kwa wanawake.

No comments:
Post a Comment