KITENDA WILI"NYUMBA YANGU NDOGO LAKINI INAENEA WATU WENGI' MBUTA NANGA!!

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO BLOG

FLORA LYIMO BLOG

FLORA

FLORA

FLORA NA RAIS JK

FLORA NA RAIS JK

FLORA NA MH PINDA

FLORA NA MH PINDA

SHINY ,HEALTHY-LOOKING AND GORGEOUS HAIR' WHATSAPP +44 778 7471024

SHINY ,HEALTHY-LOOKING AND GORGEOUS HAIR' WHATSAPP +44 778 7471024

Saturday 27 December 2014

WHATS NOW ? JE ULIISOMA HII? KUTOKA HOUSIGELI'' MPAKA KUMILIKI MADUKA'' NA HERIETH MAKWETTA''



Kutoka ‘hausigeli’ mpakakumiliki maduka London (2)
Kucheza muziki wa chakacha kulimwezesha kuishi London.
Herieth Makwetta, Mwananchi
Wiki iliyopita Flora Lyimo au Mbuta Nanga anayeishi na kufanya biashara za maduka ya nguo katika
mitaa ya Oxford inayosifika kwa kuwa na wabunifu wakubwa duniani,jijini London nchini Uingereza,
alisimulia mkasa wa maisha yake ya kutafuta mafanikio.Mbuta Nanga alielezea safari yake iliyoanzia katika Kijiji cha Kilema huko Marangu, Moshi mkoani Kilimanjaro mwaka 1989.
Alianza kwa kufanya kazi za ndani jijini Nairobi nchini Kenya na kukumbana na visa vingi, safari
hii anaelezea jinsi alivyoachana na kazi za ndani na kugeukia uchezaji chakacha. Endelea…
Mbuta Nanga anasema baada ya kukutana na wasichana wengine wanaofanya kazi za ndani,
walimshauri aingie katika uchezaji chakacha, anasema baada ya kukubaliwa maombi, aliwaomba afike Jumapili kwani ni siku ambayo hupata nafasi ya kukubaliwa kutoka na mwajiri wake.
“Nilifurahi mno, basi nikarudi nyumbani na kuanza kufikiria hiyo shoo nitakavyoicheza, mchana
wakati nipo nyumbani peke yangu dada akiwa kazini, mimi nikawa naweka muziki najichezea nyimbo za lingala ambazo nilinunua pale pale, waliniuzia nyimbo za chakacha.
Siku iliyofuata baada ya wiki moja, nikaenda na kanga mbili tu wakaniambia upo tayari nikasema
ndiyo basi wakaweka ile cd nikawa nacheza na baada ya kumaliza wakaniambia, ‘hongera sana
yaani unaweza kuliko hata huyu dada tulie naye sasa hivi’, nilifurahimno,” anasimulia Flora.
Aliambiwa kuwa ahudhurie tena wiki iliyofuata na aanze kucheza na aliambiwa kwamba angelipwa
kiasi cha shilingi mia tano kwa fedha za Kenya.“Waliniambia wangenilipa na kwamba watu watakaokuwa wakija kunitunza stejini, hizo pia zitakuwa ni pesa zangu, sikujali nikaitika
na kurudi Jumapili iliyofuata. Nikawekewa cd yangu na kutangazwa kuwa kuna mchezaji mpya
wa chakacha Flora Lyimo, nikaingia na kuanza kucheza, nilipomaliza na kurudi zangu nyumbani ni
kama sijakwenda kucheza shoo,yani yule dada ninayemfanyia kazi sikumwambia yeye wala mtu yeyote,”anasema. Anasimulia kuwa kumbe alivyokuwa anacheza alirekodiwa na jioni waajiri wake walivyokuwa wakiangalia runinga, wakamwona kwenye taarifa ya habari.“Nikiwa chumbani niliitwa
na kuulizwa, dada akaniambia kwamba nitafute pa kwenda maana haniamini na yale mauno kwa
 
MfanyabiasharaFrola Lyimo‘Mbuta Nanga’,akiwa katikaduka lake linalojulikana
kwajina la ‘FloraLyimo TZUK MBUTA NANGA’lililopo katikamitaa ya Oxford jijini London,Uingereza,
Pichakwa hisani yamissfbknitwearlyimo.blogspot.com.
MAISHA NUKUU
 “Nikiwachumbani niliitwa nakuulizwa,dada akaniambia kwamba nitafute pakwenda maana haniamini na yale mauno kwa mume wake, kaona ataanza kunitamani na hata amuache yeye, basi akanitafutia sehemunyingine nikakae na rafiki yake.”
Jinsi alivyofungua duka
Mbuta Nanga anasema hata hivyo hakuwa anatarajia kufungua katika mtaa huo wa wabunifu maarufu
duniani, bali alihisi kwamba angefungua sehemu yoyote ile.“Sikupanga kufungulia hapa,nilikuwa najipanga kwa kukusanya pesa tu maana bila kuwa na pesa huwezi kufanya chochote, nikawa pia naulizia watu wenye maduka hapa mjini mtaa wa Oxford kwa sababu nilikuwa nafanya kazi kwenye
hilo duka kubwa mtaa huu huu,” anasema Mbuta Nanga.
Anasimulia kuwa kwa kipindi chote alikuwa kipenzi cha wengi na hivyo aliweza kupata watu wa
kumwonyesha njia.“Nilikuwa naishi na watu vizuri, pia kutaka kuwajua watu na maendeleo wanafanyaje hadi wameweza kufikia walipo, ndipo siku moja nikakutana na mmoja wa wenye maduka hayo akaniambia vipi bado watafuta duka? kuna duka hapa mjini lipo wazi njoo
ukaulizie.”
Anasema hapo ndipo alipopata mwangaza, “Nikaenda kuulizia na kukuta kweli lipo na hapo hapo nikaenda kuongea na watu wa benki na wakanipa mwongozo wa biashara na ninavyohitaji kwa
hela nilizokuwa nazo, pia wataniongezea kwa malipo fulani, basi nami sikusita nikachukua mkopo
na kujazia na pesa zangu na ndipo unaona sasa hivi ninaweza kupeperusha jina langu Flora Lyimo TZUK likiambatana na MBUTA NANGA,”
anasimulia.
Nini maana ya Mbuta Nanga?“Mbuta Nanga ni kama mshangao wa kusema ‘Mungu wangu’,
kwa hiyo mimi huwa ninalizungumza sana mitandaoni kabla hata sijaanza kuitwa hivyo na watu
wengi maana vitu vyangu ninavyovifanya kwa kweli mimi mwenyewe hujisemea ‘Mbuta Nanga’,
anasema. Anasema watu wengi hata alipokodisha hilo duka humuuliza maana ya hilo jina, “Huwa nawaambia ni lenye asili ya Kichaga na maana yake ni mshangao kama ‘Oh my God’ (Munguwangu) kwa hiyo wakabakia kuanza kulisema na hata sasa hivi mjini wananiona na kusema ‘Mbuta Nanga’ hahaha”,kwa kweli ni jina ambalo limekuwa geni na la kufurahisha watu na hata mimi mwenyewe,” anasema.Mbuta Nanga anasema yeye binafsi huwa anajiuliza na kujisifu kwa hatua aliyofikia na hivyo kumwongezea morali wa kufanya kazi.“Mimi mwenyewe huwa najiuliza Flora Lyimo Mchaga Ulaya,nimefungua duka mtaa wa mapesa,yaani huu mtaa pia nimeuita mtaa wa mapesa kwa sababu ya pesa ambazo watu huja kumwagia hapa yaani kununua bidhaa hapa hakuna mtu ambaye anakuja mtaa huu umkute siyo mnunuzi wa kitu fulani, kwa hiyo pia ndiyo sababu nikauita hivyo,” anasema.
mume wake, kaona ataanza kunitamani na hata amwache yeye, basi akanitafutia sehemu nyingine nikakae na rafiki yake na mimi nikaenda kwa huyo rafiki yake na wiki iliyofuata nikaenda kucheza shoo kama kawaida na kuwaambia matatizo niliyopata wakati wao hawakuniambia kama nitatokea kwenye tv.”Flora anasema wakamtafutia chumba ili aishi peke yake suala ambalo alilifurahia sana na hapo hapo akaachana na shule na kuendelea na uchezaji wa chakacha.“Nilicheza chakacha hadi mwaka 1992 nikaenda Mombasa na wengine walionichukua ambao waliniambiakwamba huko kuna dili zaidi, tukaenda huko na nikapewa kazi ya kucheza chakacha Florida Night Club Mombasa na wakaniita Miss Florida Queen of Chakacha,”
Anasimulia.
Safari ya London yaiva
Anasimulia kuwa, maisha yaliendelea na hatimaye akafanikiwa kuwa mchezaji bora na mfano wa
kuigwa nchini Kenya, alijitahidi kuhakikisha kwamba anaifanya kazi yake ipasavyo na ilipofika
mwaka 1994 mambo yakazidi kuwa mazuri na safari ya kwenda London
ikaiva.“Nikacheza pale mpaka 1994 ndipo nikaja London kucheza shoo pia, nilipofika hapa nikawa nacheza na bendi moja ambayo nayo ilikuwa ikipiga chakacha na baada ya hapo nikaona wale watu wa bendi nao wananitaka kimapenzi nikaachana nao na kutafuta kazi za kuuza dukani,” anasimulia.
Mbuta Nanga anasema huo ndiyo ulikuwa mwanzo wake wa kufanya kazi za dukani na japokuwa
alikuwa akiendelea na uchezaji chakacha anapopata nafasi, kazi yake kubwa ilikuwa ni kuuza katika
maduka ya watu.“Nilipoona mambo yanabadilika sikukata tamaa na kurudi nyumbani, niliona nitumie fursa hiyo kujitafakari nini cha kufanya. Nikaona nianze kufanya kazi kwenye maduka
madogo madogo hadi nikaja kuajiriwa kwenye duka kubwa la mavazi yote ya watoto, wanawake
na wanaume,” anasema. Anasimulia kuwa kazi ya kuuza duka aliipenda sana, na wakati huo
alikuwa akijitahidi kujifunza namna ya kufanya biashara hiyo ili baadaye na yeye aje kuwekeza huko.
“Nilifanya nao kazi kwa muda wamiaka saba na ndiyo hapo nilipojifunzia ujuzi wa mambo ya biashara na huku nikisema siku moja na
mimi ningependa kuwa na duka la mavazi kama hili, kwa hiyo hii ni kama ndoto yangu niliyokuwa
nayo siku nyingi, baada ya miaka 39, nimefanikiwa kuitimiza,” anasimulia.

No comments:

Post a Comment