''TUMSIFUNI YESU KRISTU ''NA MAMA YETU BIKIRA MARIA''
|
FLORA LYIMO (MBUTA NANGA) MTANZANIAALISI AIPENDAE NCHI YAKE KUPITA MAELEZO ''
NDUGU ZANGU WANZANIA WENZANGU '' Nina matumaini makubwa ya kwamba HAMJAMBO POPOTE PALE MLIPO'' Vile vile nina furaha kubwa sana sana kuweza kujiona siku ya leo nimeweza kuamka salama kabisa na pia kupata nafasi yakuweza kuwaandikieni haya nitakayo waambia leo '30-5-2015 KUHUSU UKUWEPO WETU HAPA UK NA KUJISHUGHULISHA NA MAKUTANO HASA KUPITIA KANISANI '' UWE MKRISTU AU MUISLAM '' TUKUTANENI HATA JUMAPILI MOJA KWA MWEZI ILI TUWEZE KUJUANA NA VILE VILE KUBADILISHANA MAWAZO ''
''CHA MUHIM NA KUJIPANGA'' Mwajua wengi wetu wakati tunapokuwa wazima wa afya ,kazi tunayo ,mke unae,mpenzi unae,watoto unao ,maisha yako unavyopenda wewe unayo '' pesa unazo '' Wajua tunajisahau kabisa kwamba hivyo vyote TUNAWEZA KUAMKA NA KUKUTA HATUNAVYO 'Na vile vile hata kuamka pale ulipo lala Usiku unashindwa kabisa'' Yani ni jambo ambalo LIPO ''LINAWEZA KUTOKEA tena wakati wowote'' Sasa basi cha msingi na ninachotaka kuwaambieni siku ya leo ni kwamba'' Tusisubiri mpaka yatukute au yakukute'' tukumbukeni ULE MSEMO USEMAO '' (AKIBA HAIOZI) Jamani tuwe tunakutana hata mara moja kwa mwezi tukishirikiana na Wenzetu Wakenye au hata Nchi zingine kwa watakao penda'' ili Tujadiliane jinsi gani yakuweza kujisaidia wakati wa shida '' Shida kubwa kama vile MISIBA'' Ndugu zangu Wanzania wenzangu '' kama mnavyojua tunatabia hii ambayo ni kubwa sana yakusema ONA WENZETU WAKENYA WANAVYO TUSHINDA KWA VITU HIVI NA VILE ? Hebu leo tujiulize je ? ni kwanini na sisi tusiweze kufanya wafanyao hao Wenzetu wakenya au makabila mengine ? Yani kiukweli hakuna kitu wanacho kifanya wao nasi kukiona kizuri wooow wameweza ,alafu na sisi tusiweze '' TUNAWEZA KABISA'' Maana kila walichokitumia na sisi tunacho '' Kwa hiyo ni kwanini na sisi tusifanye kama wao ? Kwa mfano '' Makanisani '' Wanakutana wanasali kwa pamoja na wakimaliza wanapata chai kwa pamoja na hapo hapo kuweza kujuana na kubadilishana mawazo '' na wanafanya hivyo kila Jumapili ijayo kwa Mungu '' Sasa wewe jiulize Sisi Watanzania ni kwanini tusiweze kufanya hivyo ? na Tukawa tunafanya ya maana ,sio unahudhuria kanisani hapo kwa sababu unataka kuomba misa sijui ya Shukrani au mengineyo '' Yani tuwe tunahudhuria kwa kuomba Mungu na kuweza kubadilishana mawazo na kutoa sadaka zetu kwa Mungu alozitupa kwa pamoja na Vile vile tukaweza kukusanya Pesa kidogo hata kufungua Bank account yetu ya SHIDA'' ili tuweze kuweka huko hata £10 PAUNDI KUMI KWA KILA MWEZI '' Hiyo nadhani wengi wenu haitawashinda'' na Mimi mwenyewe Flora Lyimo ''Nipo tiyari kwa Mchango wangu na pia kusaidia kufungua hiyo Bank yetu ya ''SHIDA'' UNAWEZA KUFIWA LEO AU KESHO '' Ndugu zangu wanzania '' Hata uwe tajiri wa Dunia'' HUWEZI KABISA KUJIZIKA UKIFA LEO AU KESHO '' Na hivyo basi '' Msiwapeni ndugu zenu au familia zenu mizigo ambayo wenyewe Ukifa na utajiri wako '' Wanaanza kujisambazasambaza tena huku wakitumia Marafiki zao ili waweze kuwasambazia misaba hiyo ili wapate michango ,maana wao hawana ushirikiano mzuri na wenzao Wanzania au WALISHA SEMA HAWAJICHANGANYI 'Sasa hapo yule alokufa tajiri na mihela yake ''kumbe hata bank account ndugu hawana uwezo wakuweza kutoa chochote mle na vile vile unaweza kukuta una madeni kibao na sababu hiyo pesa zote zinazuiliwa hata usipate za kukusafirisha au kukuzika ipasavyo '' kitakacho bakia utachomwa kivuli chako kitazikwa vizuri tu kwa BURE AU BEI RAISI HAPA UK '' Ila wajua sisi wengi wetu Wakristu kuchoma watu wanapo kufa SIDHANI KAMA NI HISTORIA YETU AU NI KITU AMBACHO TUNAKIFANYA'' Mimi tangu udogo wangu hadi ukubwani nilikuja kugundua hilo la mtu kuchomwa na majivu yake sijui kuhifadhiwa sijui kwenye vikopo mara kutupwa baharini mara sijui wapi ''yani hayo yote nimeyajulia Ulaya hii'' I HATE IT'' Yani hata kwenye mazishi nikisikia ni mtu kuchomwa sipendi nijikute nimehudhuria'' I THINK NI DHAMBI KUBWA SANA TENA SANA ''NA MUNGU HAPENDI '' NA HATA ALOCHOMWA HATAKWENDA MBINGUNI '' ''NGACHOKA'' Lingine ni sasa wewe ambae hujichanganyi unaachia rafiki zako wakuchanganyie wenzako ambao wewe mwenyewe hujichanganyi nao '' waje kukutolea michango na pia kujiunga na wewe kwenye Misiba au shida zako '' Hiyo naona ni aibu na kujichora sana'' maana watu wanakusema vibaya mno japo wanatoa ile michango na pia kuja kukufariji '' KAMA UNA TABIA HII'' BADILIKA SASA NDIO MUDA WAKO /WENU /WETU wakubadilika'' Hakuna Mzungu ambae anaweza kukusaidia ukiwa na shida kivile sisi wenzako tungeweza kukusaidia'' Tusitegemee wazungu tukijua wao ndio kila kitu '' Wala tusitegemee Ubalozini kujua ndio mambo yote'' Ubalozi haupo nchini za nnje kwa kuwasaidieni kwa shida zenu au shida zetu binausi '' Yani hilo tukae tukijua kabisa'' Na kujipanga'' Mimi nawashangaa sana watu wapo bizi kushughulika na maisha ya wenzao na kuwachukia bure ,kisa wanafanya yao ili wapate kuishi wapendavyo au hata mtu anajipa raha zake kwa vile ampendavyo ''My dears'' nawe JISHUGHULISHE ,JICHANGANYE ,JIPE RAHA ZAKO UPENDAVYO WEWE'' KARIBU KANISANI APA KUJICHANGANYA' UPO /MPO EeeE'' ''AIKA RUWA'' Kila jumapili Mimi hujitahidi sana kwenda kanisani hapa hata mara moja kwa mwezi ili kujichanganya na wenzangu wa AFRICA ZAIDI '' WANYUMBANI ZAIDI ''Na pia nina kanisa langu ambalo lipo karibu na maduka yangu mjini Oxford Street ''Hilo kanisa ndilo la kwanza kuhudhuria nilipokuja London kwa mara ya kwanza kuishi mwaka 1994'' Yani kitu cha muhim nilichokitafuta ni KANISA LA ''KATOLIKI '' Niliuliza na nikaonyeshwa hili ambalo ndilo hupita pita hapo nnje karibia ya kila siku na nikisali na kumshukuru Mungu na Mama yangu Bikira Maria'' Na hapa kwenye kanisa langu mtaa wa Mapesa ni Wenzetu wa mataifa mengine na Waingereza wenyewe ndio utakutana nao kwenye hilo kanisa'' Sasa basi mwenzangu ''Pia naomba ujiamini ,ujikubali na ujue kufaham maswali kabla yakujibu ''
Kuna siku niliuliza Mtu '' Ambae pia alifiwa na Mama yake Mzazi hapa UK' na ikawa kwa ushirikiano wa Ndugu na Marafiki kukafunguliwa group kwa ajili ya mchango wa msiba huo in Whatsapp''
Basi watu wakawa wana adiwa na kukaribishwa mle wengine wakiwa hata hawamjui alofiwa wala kuwahi kumuona alokufa '' but kwa kuwa pesa zilikuwa zinahitajika kwa ajili ya mazishi '' Lazima UBINADAM ukuwepo in 100% Kushangia chochote ulichonacho''
Basi pesa zikawa bado ''watu wakawa wanatafuta namna ya kuzikamilisha'' Mimi Flora Lyimo from mawazo yangu '' Nikapost mle'' Kuuliza swali la kutaka kujua Alofariki ili niweze kuwapa ushauri mwingine ambao lengo lake ni kupata zile pesa kupita marehem''
''swali nililouliza ''
Jamani marehem alikuwa anaishi vipi hapa UK ? Nilichojibiwa na Mtu mbae sinahabari kabisa ikiwa msiba anaundugu nao au la'' ni aliropoka kama mwizi '' nakujibu '' HAYAKUHUSU ''MAISHA YA WATU WANAVYOISHI HAPA UK HAYAKUHUSU '' Jamani wajua nilitamani angeniambia hivyo in my face'' ningemzabua kofi PAAAAAAAAAAA'' alafu angepata faham''ya kwamba sijauliza watu wanavyoishi maisha yao hapa UK'' niliuliza marehem alivyokuwa anaishi hapa UK ''na ikiwa hayanihusu ''BASI MLITUHUSISHA KWENYE HILO GROUP KUTOA MISHANGO YA MAZISHI KWANINI ? Singesema hayanihusu au hayatuhusu na msituhusishe ? Yani anabahati watu walinipigia sim na kuniomba nimuache huyo ni
''le mburulaz '' hajitambui 'na maisha yake hapa UK anaishi kama mwizi tu''ndiyo sababu ''hata swali hakuweza kujibu ''karopoka mapovu yalimtokaje''
Sasa mtoto mwenye Msiba nae akanijibu ''
Hhahaha''Ngoja nicheke kidogo maana nilicheka sana''
alinijibu hivi''
Na dada yangu FLORA#Labda tu kujibu swali au hoja yako.Ni kwamba ,kama nilivyo mimi mwanae naishi hapa kama Mtanzania na mkoba wangu wa kibongo na marehemu mama naye alikuwa hivyo hivyo .Nina uhakika na hilo .2013 tulienda nyumbani pamoja na alitumia pp yake ya kibongo .Tafadhali Naombeni tuache huu mjadala wa UWEZO WA UBALOZI WETU NA MSIBA HUU.ASANTENI SANA WAPENZI.
MBUTA NANGA'' #juaswalikwanza
Hahhaa''jamani hili ndilo jibu nililijibiwa ,WEWE UNALIONAJE ? je ni sahihi ? Wacha niwafahamisheni ''
Mtu anapo kuuliza unaishije hapa UK ''? Hakuulizi kama una mikoba sijui makaratasi ''Yani Paspoti ''Hapana kabisa jamani ''Mimi sijui kama nikutokulewewa swali au nikuropoka au nikutokujiamini ''
sasa wewe mtu badala ujibu ' (kwa mfano ) Mama alikuwa anaishi hapa UK kwa muda fulani na alikuwa anafanya kazi au Biashara zake so and so Na hadi kifo chake alikuwa anaishi london na akiwa anafanya kazi au biashara zake so and so ''au alikuwa kesha acha na alikuwa nyumbani hadi kifo chake'' YANI MIMI SIKUULIZA MAMBO YA MIKOBA ''KABISA '' NA SASA MJUE NA KUJIPANGA MNAPO ULIZWA MASWALI '' MSIROPOKE KAMA WEZI NA WAKIMBIZI AU WALIOJILIPUA'' maana siku zote wanaishi kwa wasi wasi '' JUENI SWALI HILO MLILO ULIZWA NA KULIJIBU IPASAVYO '' NGACHOKA'' haahhaa'' JAMANI MIMI SIFUATILII KAMA WATU MNA MIKOBA AU ''LA'' Yani utajijua mwenyewe maana KUFA KWAJA KWA KILA MTU '' Sasa ikiwa hiyo mikoba huna ''Jipange usije ukafa ukaachia familia na ndugu zako shida maana hata hao hao marafiki wanaweza wakagoma kwa sababu unazozifaham wewe ulo fariki'' TUMSIFU YESU KRISTU ''
MY DEARS TUJICHANGANYENI NA TUJIPANGE''
UNAKARIBISHWA KILA JUMAPILI'' At Prayer Temple.119 East India Dock Road,London E14 6DE Tel. 020 7515 1616 www.ccbc.org.uk info@ccbc.org.uk |
No comments:
Post a Comment