KITENDA WILI"NYUMBA YANGU NDOGO LAKINI INAENEA WATU WENGI' MBUTA NANGA!!

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO BLOG

FLORA LYIMO BLOG

FLORA

FLORA

FLORA NA RAIS JK

FLORA NA RAIS JK

FLORA NA MH PINDA

FLORA NA MH PINDA

SHINY ,HEALTHY-LOOKING AND GORGEOUS HAIR' WHATSAPP +44 778 7471024

SHINY ,HEALTHY-LOOKING AND GORGEOUS HAIR' WHATSAPP +44 778 7471024

Sunday 16 June 2013

BY FLORA LYIMO~KWA KUSEMA KWELI WATANZANIA WENZANGU WENGI WENU HAMPENDI KUAMBIWA UKWELI'' NA HAPA OMMY DIMPOZ AMESEMA UKWELI" NA HAJAKOSEA KABISA NA WALA HAJAMTUKANA WALA KUMDHARAU MAREHEM NGWAIR"

FLORA LYIMO MTANZANIA ALISI AIPENDAE NCHI YAKE KUPITA MAELEZO" 
Huu ndio Mtizamo wangu kuhusu Hii Habari ya Wakosaji"  
Mkimsoma kimaendeleo na kumchambua  ngazi baada ya ngazi mtamuelewa kwamba Dimpoz yeye anaimanisha 'kwa pale alipo ona mwenzake Msanii Ngwair alipokufa na kifo chake kikatandazwa hadharani kwamba amefariki kwa kumega  madawa ya kulevya 'basi na yeye kwa mtizamo wake asingependa afe hivyo '' kama mnabisha alikufa Kimasikini ni mara ngapi mlimsikia Marehem amekuja majuu kupiga Nyimbo zake au hata Mmemsikia akiwa majukwani miji mbali mbali kila mwezi huko Tanzania?Isitoshe yeye alishawahi kufika mahali kama Dimpoz na kwa pale ambapo wengi pia mmeona wakizuia Nyimbo zake zisipigwe maredioni wakati alipokufa ndo hapo mtajua kwamba ni kweli alikuwa keshajichokea na Maisha yake yakubembeleza na mwisho wa siku akaamua kujiingiza kwenye umegaji wa Madawa ya kulevya na alichoambulia huko ni hasara tupu UMASKINI na hadi kumsababishia kifo chake ambacho kimemuondosha kiumasikini  na ndipo Msani mwenzake anapojaribu kusema hatapenda kufa masikini kama yeye'' na mimi pia na muunga mikono yote na miguu na akili zangu zote Asikubali kabisa kujimegea madawa ya kulevya hata kama una mipesa yako na upo juu 'lazima yatakudhuru na mwisho wasiku kufa Masikini kama wakina MICHAEL JACKSON '', WHITNEY HOUSTON NA MASTAR WASANII WENGI AMBAO TUMEWAZIKA MASIKINI NA WALISHAWAHI MPAKA KUWA MATAJIRI WAKUBWA DUNIANI'' KWA HIYO MSIROPOKE KWA WIVU JAMANI .MPENDENI DIMPOZ NA MZIDI KUMPA SUPPORT KWANI YEYE HAKUSEMA VIBAYA NI WANAOMUONEA WIVU NA CHUKI ZAO WANAZOZIJUA WENYEWE KUMPACHIKIA MANENO NA MISTARI YAO NI DHUMUNI LA KUUZA MAGAZETI AU HABARI POPOTE WAJIPATIE SHIBE NA VILE VILE HII KWAO WANAONA NI BORA KUMUARIBIA MWENZAO JINA NA KAZI YAKE KWANI WAKIUZA SEMBE (MADAWA HAYO WATAJIKUTA JELA FOR LIFE HATA NA KUNYONGWA' LAKINI KWA KUMCHAFULIA MWENZAO JINA NA KAZI YAKE WATAFUNGWA NA JELA IPI? ANYWAY KAENI MKIJUA HII DUNIA WATU WENGI WANAISHI KWA KUJIPATIA RIZIKI KUPITIA KWA WENZAO ' KWA HIYO SIYO MBAYA PIA''NYIE NUNUENI MAGAZETI NA ENDELEENI KUWAPENDA WANAOPACHIKWA HUKO AU PIA WACHUKIENI KWA YENU WENYEWE" NA SIYO KWA YALE MSOKUWA NA UHAKIKA NAYO ,,NYIE KAENI MKISOMA NA KUTIZAMENI PICHA 'ILA MSISAHAU SIYO KILA KITU UNASOMA AU UNAAMBIWA HUWA NI CHA UKWELI KAMA HUNA UHAKIKA NACHO KWA KUKISIKIA MWENYEWE AU KUKIONA MWENYEWE NA MACHO YAKO  MAWILI " MBUTA NANGA!!
JUMANNE (JUNI 11)
Kutokana na uzito wa maneno ambayo Ommy aliyatamka kuhusu Ngwair, siku iliyofuata (Jumanne), global publisher walimpigia simu kumuuliza kama maelezo hayo ya kashfa aliyatoa akiwa amelewa au la?

MOJA WA WIMBO WAKE OMMY DIMPOZ 'AMBAO UMEMUWEKA JUU '' NA KAMA ATAANZA KUMEGA MADAWA YA KULEVYA NA KUTOKUJUA WAJIBU WAKE NA KUIPENDA KAZI YAKE BASI MSISHANGAE MKIMKUTA STENDI AKISEMA FANYA FASTA FASTA ..DAR MPAKA MOSHI 'MBUTA NANGA'' NDIYO MAANA ANASEMA HAPENDI AFE MASIKINI '''SO STAY AWAY FROM DRUG MY DEAR'' I JUST LOVE MAENDELEO YA WATANZANIA WENZANGU'TUPENDANE NA TUINUANE KWENYE BIASHARA ZETU" JUST ME AND YOU...I LOVE HUU WIMBO KINOMA'' BE BLESS AND GOD BLESS TANZANIA AND R.I.P. NGWAIR''

HEBU WASOME APA"

Ommy kwa kujiamini, alijibu kwamba alichokisema kuhusu Ngwair ni ukweli kwa asilimia 100.
MWANDISHI: Nakushauri kama mdogo wangu, siku nyingine usirudie kutamka maneno hayo ni mabaya sana kwa mtu aliyekufa.
OMMY: Sijaongea neno baya, nimesema ukweli wasanii hatutakiwi kufa maskini.
MWANDISHI: Wewe unaona mtu akichangiwa baada ya kufa ndiyo kipimo cha umaskini?
OMMY: Kuna mambo mengi ambayo yangefanyika kabla ya kuchangiwa lakini Ngwair alishindwa kuyafanya.
MWANDISHI: Sasa Ngwair angefanya nini wakati yeye ameshakufa?
OMMY: Kuna mambo yangefanyika, mfano kusafirisha mwili kutoka Afrika Kusini.
MWANDISHI: Sasa Ngwair angejisafirisha mwenyewe?
OMMY: Nachosema mimi ni kwamba wasanii hatutakiwi kufa maskini.
MWANDISHI: Sikiliza Ommy, hata mabilionea wakubwa huwa wanachangiwa. Mtu kuchangiwa siyo kashfa wala aibu kama unavyotaka kulionesha tukio la Ngwair. Marehemu Steven Kanumba alikuwa anatembelea Toyota Lexus V8, mbona alipokufa kila kitu alifanyiwa? Ni jambo la kawaida.
OMMY: Ngwair alikuwa na ‘stresi’ za maisha ndiyo maana alikuwa anakula unga.
MWANDISHI: Ulishawahi kumwona Ngwair akitumia unga?
OMMY: Kwanza nakusikia unanirekodi, sijui una malengo gani.
MANENO YA KASHFA MLIMANI CITY
Juni 8, mwaka huu, katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, wakati wa utoaji wa Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA)  mwaka 2012-2013, Ommy Dimpoz alizungumza maneno ya kashfa ambayo moja kwa moja yalitafsiriwa ni dongo kwa Ngwair.
Baada ya kutangazwa mshindi wa kipengele cha Video Bora ya Mwaka na kukabidhiwa tuzo yake, Ommy alibwabwaja: “Jamani tumechoka kuzika wasanii maskini wenye majina makubwa.”
Japo hakutaja jina la yule aliyekuwa anamzungumzia, tafsiri ya wengi ni kwamba Ommy alikuwa anamzungumzia Ngwair kwa sababu ndiye staa aliyekuwa amezikwa kishindo cha siku moja tu kabla ya usiku huo wa tuzo. Ngwair alizikwa Alhamisi, tuzo Jumamosi.
“Huyu dogo ana nyodo sana, sasa haya ni maneno gani ya kuzungumza? Hapa anamzungumzia Ngwair, ila anapaswa kujua kwamba yeye bado msanii mdogo sana kumlinganisha na Ngwair,” alisema mtangazaji mmoja kwa masikitiko.
MAPOZI NI KAWAIDA YAKE, ATIMULIWA KIGOMA ALL STARS
Ndani ya Kampuni ya Kigoma All Stars, awali Ommy alikuwa mmoja wa wajumbe kwenye bodi ya wakurugenzi lakini hivi karibuni alitimuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Peter Msechu.
Chanzo chetu makini ndani ya Kigoma All Stars, kimetonya kuwa Ommy alionesha tabia mbaya dhidi ya wasanii wenzake wanaounda kampuni hiyo, hivyo hakukuwa na jinsi zaidi ya kumtimua ujumbe wa bodi na kumuweka Msechu.
“Alikuwa ameshakuwa kero. Unajua pale Kigoma All Stars wote ni mastaa lakini yeye anajiona yupo juu ya wote. Tunaitisha vikao hatokei, tunakwenda kufanya shoo hatokei, tunamuona hana umoja na sisi na hatufai.
“Uamuzi wa kwanza ulikuwa ni kumtimua kabisa ili asiwepo kabisa kwenye kampuni yetu, maana siyo lazima kila mtu mwenye asili ya Kigoma awepo Kigoma All Stars. Baadaye kwa busara za mlezi wa kampuni yetu, Zitto Kabwe ndiyo tukamuondoa kwenye bodi.
“Tumembakiza kwenye kampuni kama mwanahisa wa kawaida tukiwa tunampima. Akiendelea kuleta mapozi yake, hatutamvumilia, tutamfukuza moja kwa moja,” kilisema chanzo chetu.
Chanzo hicho kiliongeza, ndani ya Kigoma All Stars kuna wasanii wakubwa kama Nasibu Abdul ‘Diamond’, Ali Kiba, Mwasiti Almasi, Sunday Mangu ‘Linex’, Banana Zorro na wengineo lakini hawaringi, isipokuwa Ommy ndiye fungakazi kwa maringo.
Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), vilevile Waziri Kivuli wa Fedha na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alipoulizwa kuhusu Ommy kutimuliwa kwenye bodi, alikiri hilo kufanyika.
“Ni kweli kuna mabadiliko kwenye bodi, wanamuziki wenyewe kwa sababu ndiyo wanahisa, waliamua kumuondoa Ommy Dimpoz na nafasi yake akawekwa Peter Msechu,” alisema Zitto.
Kuhusu kutimuliwa kwenye bodi Kigoma All Stars, Ommy hakutaka kuzungumza chochote, badala yake alijikanyagakanyaga.

OMMY NA NYIMBO TATU
Ommy anajiita super handsome, mapozi, kampuni yake anaiitwa Pozi Kwa Pozi, majina hayo yanatosha kueleza sababu kwa nini amemdhihaki Ngwair na haelewani na wasanii wenzake.
Ndiyo kwanza ana nyimbo tatu tu, Nai Nai (alisaidiwa sana na Ali Kiba), Baadaye na Me & You (amesaidiwa sana na Vanessa Mdee) lakini amekuwa wa migogoro na mbwembwe nyingi dhidi ya wasanii wenzake.
Alishawahi kurushiana maneno kwenye vyombo vya habari na mwanamuziki Cyril Kamikaze, baadaye akaingia kwenye gogoro zito na mwana Hip Hop wa Nako 2 Nako Soldier, Isaac Waziri Makuto ‘Lord Eyez’.
Kuhusu Lord Eyez ambaye ni memba wa Familia ya Weusi, alidai alimuibia taa, power windows, vioo na vifaa vingine vya gari lake lakini kesi ilipofika mahakamani, Ommy hakwenda kutoa ushahidi.
Ommy alishindwa kutoa ushahidi lakini kabla yake alitangaza katika vyombo vya habari kuwa Lord Eyez ni mwizi na kwamba alimwibia vifaa vya gari lake, zaidi ya hapo alikusanya watu wakampa kipigo memba huyo wa Weusi kisha wakampeleka polisi ambako aliwekwa lupango.

1 comment:

  1. Dada Flora Bahati Lyimo 'haujambo '' yani hii ndiyo sababu tunakupenda kwa maukweli yako..nilikuwa nasubiria kuona utakavo jibu' na umejibu kiukweli kabisa hata mimi sikuona alipokosea Ommy Dimpoz au alipomtusi Ngwea ,,na huo mfano wako wa Michael na Whitney ni mfano mzuri sana,asante na Mungu azidi kukubariki..Mdau wako "

    ReplyDelete