JUMANNE (JUNI 11)
Kutokana na uzito wa maneno ambayo Ommy aliyatamka kuhusu Ngwair, siku iliyofuata (Jumanne), global publisher walimpigia simu kumuuliza kama maelezo hayo ya kashfa aliyatoa akiwa amelewa au la?
MOJA WA WIMBO WAKE OMMY DIMPOZ 'AMBAO UMEMUWEKA JUU '' NA KAMA ATAANZA KUMEGA MADAWA YA KULEVYA NA KUTOKUJUA WAJIBU WAKE NA KUIPENDA KAZI YAKE BASI MSISHANGAE MKIMKUTA STENDI AKISEMA FANYA FASTA FASTA ..DAR MPAKA MOSHI 'MBUTA NANGA'' NDIYO MAANA ANASEMA HAPENDI AFE MASIKINI '''SO STAY AWAY FROM DRUG MY DEAR'' I JUST LOVE MAENDELEO YA WATANZANIA WENZANGU'TUPENDANE NA TUINUANE KWENYE BIASHARA ZETU" JUST ME AND YOU...I LOVE HUU WIMBO KINOMA'' BE BLESS AND GOD BLESS TANZANIA AND R.I.P. NGWAIR''
HEBU WASOME APA"
Ommy kwa kujiamini, alijibu kwamba alichokisema kuhusu Ngwair ni ukweli kwa asilimia 100.
MWANDISHI: Nakushauri kama mdogo wangu, siku nyingine usirudie kutamka maneno hayo ni mabaya sana kwa mtu aliyekufa.
OMMY: Sijaongea neno baya, nimesema ukweli wasanii hatutakiwi kufa maskini.
MWANDISHI: Wewe unaona mtu akichangiwa baada ya kufa ndiyo kipimo cha umaskini?
OMMY: Kuna mambo mengi ambayo yangefanyika kabla ya kuchangiwa lakini Ngwair alishindwa kuyafanya.
MWANDISHI: Sasa Ngwair angefanya nini wakati yeye ameshakufa?
OMMY: Kuna mambo yangefanyika, mfano kusafirisha mwili kutoka Afrika Kusini.
MWANDISHI: Sasa Ngwair angejisafirisha mwenyewe?
OMMY: Nachosema mimi ni kwamba wasanii hatutakiwi kufa maskini.
MWANDISHI: Sikiliza Ommy, hata mabilionea wakubwa huwa wanachangiwa. Mtu kuchangiwa siyo kashfa wala aibu kama unavyotaka kulionesha tukio la Ngwair. Marehemu Steven Kanumba alikuwa anatembelea Toyota Lexus V8, mbona alipokufa kila kitu alifanyiwa? Ni jambo la kawaida.
OMMY: Ngwair alikuwa na ‘stresi’ za maisha ndiyo maana alikuwa anakula unga.
MWANDISHI: Ulishawahi kumwona Ngwair akitumia unga?
OMMY: Kwanza nakusikia unanirekodi, sijui una malengo gani.
MANENO YA KASHFA MLIMANI CITY
Juni 8, mwaka huu, katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, wakati wa utoaji wa Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) mwaka 2012-2013, Ommy Dimpoz alizungumza maneno ya kashfa ambayo moja kwa moja yalitafsiriwa ni dongo kwa Ngwair.
Baada ya kutangazwa mshindi wa kipengele cha Video Bora ya Mwaka na kukabidhiwa tuzo yake, Ommy alibwabwaja: “Jamani tumechoka kuzika wasanii maskini wenye majina makubwa.”
Japo hakutaja jina la yule aliyekuwa anamzungumzia, tafsiri ya wengi ni kwamba Ommy alikuwa anamzungumzia Ngwair kwa sababu ndiye staa aliyekuwa amezikwa kishindo cha siku moja tu kabla ya usiku huo wa tuzo. Ngwair alizikwa Alhamisi, tuzo Jumamosi.
“Huyu dogo ana nyodo sana, sasa haya ni maneno gani ya kuzungumza? Hapa anamzungumzia Ngwair, ila anapaswa kujua kwamba yeye bado msanii mdogo sana kumlinganisha na Ngwair,” alisema mtangazaji mmoja kwa masikitiko.
MAPOZI NI KAWAIDA YAKE, ATIMULIWA KIGOMA ALL STARS
Ndani ya Kampuni ya Kigoma All Stars, awali Ommy alikuwa mmoja wa wajumbe kwenye bodi ya wakurugenzi lakini hivi karibuni alitimuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Peter Msechu.
Chanzo chetu makini ndani ya Kigoma All Stars, kimetonya kuwa Ommy alionesha tabia mbaya dhidi ya wasanii wenzake wanaounda kampuni hiyo, hivyo hakukuwa na jinsi zaidi ya kumtimua ujumbe wa bodi na kumuweka Msechu.
“Alikuwa ameshakuwa kero. Unajua pale Kigoma All Stars wote ni mastaa lakini yeye anajiona yupo juu ya wote. Tunaitisha vikao hatokei, tunakwenda kufanya shoo hatokei, tunamuona hana umoja na sisi na hatufai.
“Uamuzi wa kwanza ulikuwa ni kumtimua kabisa ili asiwepo kabisa kwenye kampuni yetu, maana siyo lazima kila mtu mwenye asili ya Kigoma awepo Kigoma All Stars. Baadaye kwa busara za mlezi wa kampuni yetu, Zitto Kabwe ndiyo tukamuondoa kwenye bodi.
“Tumembakiza kwenye kampuni kama mwanahisa wa kawaida tukiwa tunampima. Akiendelea kuleta mapozi yake, hatutamvumilia, tutamfukuza moja kwa moja,” kilisema chanzo chetu.
Chanzo hicho kiliongeza, ndani ya Kigoma All Stars kuna wasanii wakubwa kama Nasibu Abdul ‘Diamond’, Ali Kiba, Mwasiti Almasi, Sunday Mangu ‘Linex’, Banana Zorro na wengineo lakini hawaringi, isipokuwa Ommy ndiye fungakazi kwa maringo.
Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), vilevile Waziri Kivuli wa Fedha na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alipoulizwa kuhusu Ommy kutimuliwa kwenye bodi, alikiri hilo kufanyika.
“Ni kweli kuna mabadiliko kwenye bodi, wanamuziki wenyewe kwa sababu ndiyo wanahisa, waliamua kumuondoa Ommy Dimpoz na nafasi yake akawekwa Peter Msechu,” alisema Zitto.
Kuhusu kutimuliwa kwenye bodi Kigoma All Stars, Ommy hakutaka kuzungumza chochote, badala yake alijikanyagakanyaga.
OMMY NA NYIMBO TATU
Ommy anajiita super handsome, mapozi, kampuni yake anaiitwa Pozi Kwa Pozi, majina hayo yanatosha kueleza sababu kwa nini amemdhihaki Ngwair na haelewani na wasanii wenzake.
Ndiyo kwanza ana nyimbo tatu tu, Nai Nai (alisaidiwa sana na Ali Kiba), Baadaye na Me & You (amesaidiwa sana na Vanessa Mdee) lakini amekuwa wa migogoro na mbwembwe nyingi dhidi ya wasanii wenzake.
Alishawahi kurushiana maneno kwenye vyombo vya habari na mwanamuziki Cyril Kamikaze, baadaye akaingia kwenye gogoro zito na mwana Hip Hop wa Nako 2 Nako Soldier, Isaac Waziri Makuto ‘Lord Eyez’.
Kuhusu Lord Eyez ambaye ni memba wa Familia ya Weusi, alidai alimuibia taa, power windows, vioo na vifaa vingine vya gari lake lakini kesi ilipofika mahakamani, Ommy hakwenda kutoa ushahidi.
Ommy alishindwa kutoa ushahidi lakini kabla yake alitangaza katika vyombo vya habari kuwa Lord Eyez ni mwizi na kwamba alimwibia vifaa vya gari lake, zaidi ya hapo alikusanya watu wakampa kipigo memba huyo wa Weusi kisha wakampeleka polisi ambako aliwekwa lupango.
MBUTA NANGA!HII BLOG-MAGAZINE INASHUGHULIKA ZAIDI NA YAFUATAYO '' WALE WACHAFUAJI WA SHUGHULINI KAMA VILE HARUSINI WASOFUATA ZILE DRESS CODE' RED CARPET AND ALL OTHER EVENTS 'ALSO YOUR OLD AND NEW PHOTO'S ALL KIND OF NEWS AROUND THE WORLD & FLORA LYIMO TZUK DESIGNS &TRADES'MBUTA NANGA LONDON KARIBUNI AT MY SHOPS CALL /WHATSAP (+ 44)07787471024:EMAIL:flo1974@btinternet.com FOLLOW INSTAGRAM> mbutanangablog or MBUTANANGASTYLE
KITENDA WILI"NYUMBA YANGU NDOGO LAKINI INAENEA WATU WENGI' MBUTA NANGA!!
FLORA LYIMO TZUK
FLORA LYIMO TZUK
KWA URAHISI ZAIDI PATA KILA KITU AMBACHO KIMEPOSTIWA TANGU KUANZISHWA KWA BLOG HII
- April 2017 (1)
- March 2017 (2)
- February 2017 (2)
- January 2017 (15)
- December 2016 (8)
- October 2016 (2)
- September 2016 (9)
- May 2016 (2)
- April 2016 (2)
- March 2016 (1)
- February 2016 (4)
- January 2016 (7)
- December 2015 (10)
- November 2015 (1)
- October 2015 (1)
- September 2015 (2)
- August 2015 (13)
- July 2015 (10)
- June 2015 (12)
- May 2015 (14)
- April 2015 (3)
- March 2015 (11)
- February 2015 (33)
- January 2015 (30)
- December 2014 (36)
- November 2014 (34)
- October 2014 (29)
- September 2014 (12)
- August 2014 (56)
- July 2014 (49)
- June 2014 (76)
- May 2014 (81)
- April 2014 (73)
- March 2014 (48)
- February 2014 (39)
- January 2014 (35)
- December 2013 (81)
- November 2013 (86)
- October 2013 (112)
- September 2013 (91)
- August 2013 (119)
- July 2013 (112)
- June 2013 (124)
- May 2013 (91)
- April 2013 (119)
- March 2013 (128)
- February 2013 (119)
- January 2013 (71)
- December 2012 (1)
- November 2012 (53)
- October 2012 (76)
- September 2012 (120)
- August 2012 (58)
- July 2012 (74)
- June 2012 (109)
- May 2012 (127)
- April 2012 (140)
- March 2012 (112)
- February 2012 (214)
- January 2012 (98)
- December 2011 (168)
- November 2011 (108)
- October 2011 (107)
- September 2011 (127)
- August 2011 (225)
- July 2011 (270)
- June 2011 (218)
- May 2011 (226)
- April 2011 (208)
- March 2011 (188)
- February 2011 (94)
- January 2011 (114)
FLORA LYIMO BLOG
FLORA
FLORA NA RAIS JK
FLORA NA MH PINDA
SHINY ,HEALTHY-LOOKING AND GORGEOUS HAIR' WHATSAPP +44 778 7471024
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Dada Flora Bahati Lyimo 'haujambo '' yani hii ndiyo sababu tunakupenda kwa maukweli yako..nilikuwa nasubiria kuona utakavo jibu' na umejibu kiukweli kabisa hata mimi sikuona alipokosea Ommy Dimpoz au alipomtusi Ngwea ,,na huo mfano wako wa Michael na Whitney ni mfano mzuri sana,asante na Mungu azidi kukubariki..Mdau wako "
ReplyDelete