KITENDA WILI"NYUMBA YANGU NDOGO LAKINI INAENEA WATU WENGI' MBUTA NANGA!!

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO TZUK

FLORA LYIMO BLOG

FLORA LYIMO BLOG

FLORA

FLORA

FLORA NA RAIS JK

FLORA NA RAIS JK

FLORA NA MH PINDA

FLORA NA MH PINDA

SHINY ,HEALTHY-LOOKING AND GORGEOUS HAIR' WHATSAPP +44 778 7471024

SHINY ,HEALTHY-LOOKING AND GORGEOUS HAIR' WHATSAPP +44 778 7471024

Sunday 9 November 2014

WHATS NOW ? BREAKING NEWS'' HIVI SASA MISS TANZANIA 2014 NI LILIAN KAMANZIMA''' HONGERA SANA'' JE WATANZANIA WENZANGU MME MKUBALI ? MBUTA NANGA'' SASA WEWE SITTI MTEMVU''UJIFUNZE KUSEMA UKWELI .HII NI DUNIA YA .COM

NINI KILIKUCHELEWESHA ? MBUTA NANGA''




Aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu katika pozi na mshindi wa pili, Lillian Kamazima (kulia) pamoja na mshindi wa tatu, Jihhan Dimachk.

Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu amejivua taji hilo leo, mshindi wa pili, Lillian Kamazima amrithi, Lundenga athibitisha. Habari kamili endelea kusoma chini (click read more).


Sitti Abas Mtemvu amelivua taji hilo baada ya kuiandikia barua Kamati ya Miss Tanzania, November 5 mwaka huu, kuhusiana na uamuzi wake huo.
Mrembo huyo alikuwa akikabiliwa na shutuma za kudanganya umri wake, jambo ambalo lilililazimu Baraza la Sanaa la Taifa, (Basata) kutokana na agizo la wizara  husika kufuatilia ukweli wake.
“Baada ya kutwaa taji la urembo la Miss Tanzania kumezuka shutuma mbalimbali dhidi yangu. Wameniwekea maneno mengi sana mdomoni kwamba nimesema wakati siyo,” amesema kwenye barua hiyo.




Miss Tanzania aliyechukua nafasi ya Sitti Mtemvu, Lilian Kamanzima.

“Shutuma hizo zimeandikwa katika vyombo mbalimbali vya habari, blogs na mitandao ya kijamii, kiasi ambacho naweza hata kuhatarisha maisha yangu. Sasa kwa hiari yangu tena bila kushawishiwa na mtu na kwa kulinda heshima yangu na familia yangu natamka rasmi kuvua taji la urembo la Miss Tanzania 2014,” ameongeza.

“Napenda niwashukuru wale wote waliokuwa wakinipa sapoti tangu mwanzo nilipoingia katika mashindano haya katika ngazi ya taifa, na warembo wote wa Chang’ombe, Temeke pamoja na wote tuliokuwa nao katika fainali za Taifa. Pia napenda kutuma shukrani za dhati kwa waandaji wote wa kituo cha Chang’ombe, Temeke na wajumbe wa Kamati ya Miss Tanzania kwa mafunzo mbalimbali niliyopata. Nawashukuru pia waandishi wote kwa mchango wenu, pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo na Baraza la Sanaa kwa busara zenu.”



 Aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu katika pozi. 

“Leo nalivuta taji rasmi nililopewa na binadamu lakini alilonipa mwenyezi Mungu bado ninalo. Mwisho naomba radhi Watanzania wote kwa uamuzi huo niliochukua.”
Nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa mshindi wa pili, Lilian Kamanzima.
ASANTE KWA HABARI NA PICHA MRUSHAJI ''

No comments:

Post a Comment